Na Mwandishi Wetu, Gazetini
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limemkamata Rauli Mahabi kwa tuhuma za kumjeruhi Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania(TEC), Padri Charles Kitima.
Kwa mujibu wa taarifa ya Polisi ilitolewa na Kamanda Jumanne Muliro leo Alhamisi Mei 1, 2025, majira ya saa nne usiku wa Aprili 30,2025 ilipokelewa taarifa ya kujeruhiwa kwa Padri huyo.


Inadaiwa kuwa Padri Kitima tangu saa tatu asubuhi alikuwa na kikao cha viongozi wa dini mbalimbali na baada ya kumaliza saa moja jioni alikwenda kantini ambapo aliendelea kupata kinywaji hadi saa nne na robo usiku, alipokwenda maliwatoni pembeni ya kantini hiyo ndipo alishambuliwa kichwani na kitu butu na watu wawili.