3.6 C
New York

Mnyama achezea kichapo kingine Ligi ya Mabingwa Afrika

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

SIMBA imepoteza mchezo wa pili wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa na Stade Malien ugenini nchini Mali.

Mchezo huo uliopigwa leo Novemba 30, 2025 unaifanya Simba kupoteza mechi ya pili mfululizo baada ya mchezo uliopita kufungwa nyumbani na Petro de Luanda ya Angola 1-0 kwenye dimba la Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Matokeo hayo yanawafanya Wanamsimbazi hao kuburuza mkia katika kundi D, likiongozwa na Petro de Luanda ikiwa na alama 4, sawa na Stade Malien, nafasi ya tatu ni Esperance ina pointi 2. Kila mmoja amecheza mechi mbili.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img