3.2 C
New York

Mabondia kutishiana kabla ya Desemba 26

Published:

Na Winfrida Mtoi, Gazetini

KUELEKEA pambano kubwa la kufunga mwaka maarufu ‘Boxing On Boxing Day, tayari mabondia wanaopanda ulingoni siku hiyo wakiongozwa na Hassan Mwakinyo, wameanza kupigana mkwara kila mmoja akiahidi kumdunda mpinzani wake.

Pambano hilo linakusanya mabondia kutoka mikoa tofauti, linatarajiwa kufanyika Desemba 26,2025 kwenye ukumbi wa  WareHouse, Masaki jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa mabondia walijitokeza kuchimba mkwara ni  bondia Ally Ngwando  wa Manzese na Mussa Makuka wa Mbagala ambao siku hiyo watazichapa  kudhirishia mashabiki wao kuwa nani mkali.

Ngwando amesema yupo katika maandalizi makubwa kuhakikisha  anaweka heshima  kwa kumpa kichapo kikali mpinzani wake ambaye amekuwa akiongeza sana bila kujua kuwa mchezo wa ngumi ni vitendo ulingoni.

“Mimi nasema ajipange aje, kama anataka kuwadhirishia Watanzania aje kuonesha anachokitaka ila namwambia Makuka wewe fanya mazoezi vizuri kazi unayo, mimi sina ya kuongea sana, mikono ndiyo itakayoongea,” ametamba Ngwando.

Naye Makuka amejibu kwa kusema mpinzani wake ni bondia mwenye uwezo mdogo na siku hiyo ajiandae kukutana na chuma cha Mjerumani.

“Mimi nacheza na yoyote yule ambaye anachezea mikono, nadhani mwenyewe shahidi unanijua vizuri na unaona kazi yangu. Yaani mimi sio mnyonge kazini kwangu ndiyo kuna kazi,” amejinasibu Makuka.

Kwa upande wake bondia Osama Alabi wa Mtwara amejigamba kutwanga kwa TKO Ally Mazome kutoka Morogoro na kuweka historia ya pekee kwa mashabiki zake.

“Kijana wao niko fiti kumkabili mpinzani wangu Ally Mazome, kikubwa ni dua ili kufika Desemba 26. Hakuna asiye mjua Osama Korosho maandalizi yangu yamekuwa makubwa mno,” amepiga mkwara bondia huyo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img