22.9 C
New York

Chart| Mwenendo wa wanyamapori kuingia kwenye makazi ya watu

Published:

Na Faraja Masinde, Gazetini

Takwimu za Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA)zinaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko la matukio ya wanyamapori kuingia kwenye makazi ya watu mwaka hadi mwaka huku moja ya sababu ikiwa ni watu kujenga makazi kwenye mapito(shoroba) ya wanyamapori.

Kuwapo kwa mwingiliano huo kumekuwa kukisababisha athari kwa binadamu na wanyamapori ikiwemo kuharibiwa kwa mazao, watu kujeruhiwa, kuuawa na wanyama hao na pia kubadilika kwa tabia za wanyamapori.

Akifafanua zaidi hivi karibuni Mjini Bagamoyo mkoani Pwani wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu migongano kati ya binadamu na wanyamapori yaliaandaliwa na Chama Cha Waandishi wa Habari za mazingira Tanzania (JET) kwa ufadhili wa Mradi wa Kupunguza Migogoro Baina ya Binadamu na Wanyamapori Tanzania, unaotekelezwa na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) kwa niaba ya Serikali ya Ujerumani(BMZ).

Afisa Uhifadhi kutoka TAWA anayesimamia udhibiti wa wanyama wakali na waharibifu, Isaack Chamba anasema kuwa migongano kati ya binadamu na wanyamapori ni ya kihistoria na ilikuwa ikishughulikiwa na Idara ya Wanyamapori katika Wizara ya Maliasili na Utalii na baada ya kuanzishwa kwa Tawa, ikabeba jukumu hilo.

Amesema takwimu za Tawa zinaonyesha kwamba mwaka 2016/17 kulikuwa na matukio 833 ambapo mwaka 2017/18 yaliongezeka hadi kufikia 997 na mwaka uliofuata wa 2028/19 yaliongezeka zaidi hadi kufikia 1510.

“Mwaka 2019/20, matukio ya wanyama kuingia kwenye makazi ya watu yalipungua kidogo hadi kufikia 1426, mwaka 2020/21 yalifika 1706 na mwaka 2021/22 yalikuwa 2304 na mwaka 2022/23 yalikuwa 2817,” amesema Chamba.

Chamba anabainisha kuwa ongezeko wa matukio hayo ni sawa na wastani wa asilimia 23.76 kwa mwaka wakati uharibifu wa mazao pia ukiwa ni ongezeko la wastani wa asilimia 118.1 kwa mwaka.

Mwaka 2018 kulikuwa na ongezeko kubwa la matukio ya migongano. Ongezeko hilo liliisukuma Wizara ya Maliasili na Utalii kuandaa Mkakati wa Taifa wa Kusimamia Migongano kati ya Binadamu na Wanyamapori (2020 – 2024).

“MKAKATI HUO ULIZINDULIWA OKTOBA 5, 2020 NA UNATEKELEZWA NA TAWA, TANAPA (MAMLAKA YA HIFADHI ZA TAIFA), NCAA (MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO), TFS (WAKALA WA MISITU TANZANIA), TAWIRI (MAMLAKA YA UTAFITI WA WANYAMAPORI) NA WADAU WENGINE,” .Chamba.

“Mkakati huo ulizinduliwa Oktoba 5, 2020 na unatekelezwa na Tawa, Tanapa (Mamlaka ya Hifadhi za Taifa), NCAA (Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro), TFS (Wakala wa Misitu Tanzania), Tawiri (Mamlaka ya Utafiti wa Wanyamapori) na wadau wengine,” amesema Chamba.

Kulingana na Chamba hadi sasa wilaya 44 zinakabiliwa na changamoto ya wanyamapori kuingia kwenye makazi ya watu na kusababisha uharibifu wa mazao, mali, kujeruhi na hata kusababisha vifo kwa binadamu au wanyama wenyewe kuuawa na wananchi.

MWAKAMATUKIO
2016/17833
2017/18997
2018/191,510
2019/201,426
2020/211,706
2021/222,304
2022/232,817

Baadhi ya wilaya zinazokabiliwa na changamoto hiyo ni pamoja na Busega, Kilosa, Meatu, Nachingwea, Rufiji, Lindi, Manyoni, Itilima, Tunduru na Bunda huku asilimia 80 ya matukio yakifanywa na Tembo na kiwango kilichobaki wakiwa ni simba, fisi na nyani.

Kwa mujibu wa mtaalamu huyo, mambo yanayosababisha migongano hiyo kuwa ni pamoja na watu kujenga makazi kwenye shoroba za wanyamapori, kukosekana kwa mpango bora ya matumizi ya ardhi, mifugo kuingia kwenye hifadhi, mabadiliko ya tabianchi na kupuuzwa kwa ushauri wa wataalamu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img