1.6 C
New York

Visual| Changamoto lukuki TPA ikifikia ufanisi 2023

Published:

Na Faraja Masinde, Gazetini

Ukosefu wa Magati yanayotosheleza ikiwamo miundombinu isiyotosheleza ya reli na barabara ni moja ya sababu zinazokwamisha bandari ya Dar es Salaam kushindwa kufikia ufanisi wake kama wengi wanavyotamani kuona ikifanikiwa na kuleta manufaa kwa Watanzania.

Kulingana na Ripori ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Plasduce Mbossa aliyoitoa Januari 9, 2024, inabainisha kuwa pamoja na TPA kufikia ufanisi mkubwa kwa mwaka 2023 katika maeneo mengi, lakini bado kuna changamoto ambazo iwapo kama zingetatuliwa basi eneo la Bandari hususan ya Dar es Salaam basi lingekuwa ni kati ya machache yanayostawisha uchumi wa Tanzania kwa kiwango cha juu.

Mbossa alisema nini?

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, Bandari ya Dar es Salaam ina magati 12 ambayo yametengwa kwa ajili ya kuhududmia shehena za magari, kichele, makasha na mizigo mchanganyiko? hii ina maana kwamba miundombinu iliyopo katika bandari hiyo ina uwezo wa kuhudumia leli 12 pekee kwa wakatio mmoja.

“Hatua hii ya uchache wa magati pamoja na vitendea kazi inaendelea kuathiri utendaji kazi wa Bandari y Dar es Salaam, tatizo huwa kubwa zaidi na kuonekana kipindi cha msimu mkubwa wa shughuli za bandari(High Seasons) ambacho ni kuabnzia Septemba hadi mwanzoni mwa Februari,” anasema Mbossa.

Hii ni sawa na kusema kwamba kwa kipindi hiki chenye shehena kubwa, serikali inapoteza fedha nyingi kutokana na magati kuwa machache.

Aidha, Mbossa anaitaja changamoto nyingine kuwa ni uwepo wa miundombinu isiyotosheleza ya reli na barabara ambayo ingerahisisha uondoshaji wa shehena bandarini kwa haraka pamoja na kuharibika kwa mitambo ya kuhudumia shehena.

“Kutokana na uchakavu wa mitambo ya kuhudumia makasha, kumekuwa na changamoto ya kuharibika mara kwa mara kwa mitalbo hiyo ambayo ni muhimu katika kuhudumia meli za makasha(makontena) hatua inayoshusha tija na kuchagiza kuchelewa kutoka kwa meli katika magati,” anasema Mbossa.

Hizi ni changamoto ambazo serikali hainabudi kuzifanyia kazi katika kuhakikisha kuwa ufanisi wa bandari nchini unaongezeka na kufanya nyanja hiyo kuwa neema kwa nchi.

Mafanikio

Hata hivyo pamoja na changamoto hizo yapo pia mafanikio albayo yameweza kufikiwa na TPA kama alivyobainisha Mbiossa kupitia ripoti hiyo.

“Katika kipindi cha Julai hadi Desemba, 2023, TPA ilijiwekea lengo la kuhudumia meli 792 na hadi kufikia Desemba, 2023 ilikuwa imevuka lengo na kuhudumia meli 979 sawa na asilimia 123.6.

“Kwa upande wa ukubwa wa meli zilizohudumiwa, TPA ilikuwa na lengo la kuhudumia meli zenye ukubwa wa tani 15,576,000 katika kipindi cha Julai hadi Desemba mwaka 2023 ambapo hadi kufikia mwezi Desemba, 2023, TPA ilikuwa tayari imehudumia meli zenye ukubwa wa kiasi cha tani 17,200,692 sawa na asilimia 110.4,” amebainisha Mbossa.

Amesema TPA ilikuwa na lengo la kuhudumia kiasi cha tani 10,993,000 katika bandari ya Dar es Salaam na hadi kufikia Desemba, mwaka jana ilihudumia tani 12,052,682 sawa na asilimia 109.6 za lengo.

Mbossa amesema katika kipindi hicho, TPA iliweza kuhudumia kiasi cha makontena 509,594 sawa na asilimia 102.8 za lengo lililowekwa la kuhudumia kiasi cha makontena 495,600 kwa kipindi cha Julai hadi Desemba, 2023.

Zaidi angalia mafanikio na changamoto za TPA kwa mwaka 2023 kwenye usanifu wetu hapo juu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img