3.2 C
New York

Visual| Ushamiri wa VVU Tanzania

Published:

Na Faraja Masinde, Gazetini

Ripoti mpya ya Utafiti wa Viashiria vya UKIMWI nchini Tanzania inaonesha maambukizi mapya miongoni mwa watu wazima wenye umri zaidi ya miaka 15 yanaendelea kupungua.

Kulingana na ripoti hiyo iliyozinduliwa Desemba 1, 2023 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, maambukizi mapya miongoni mwa watu wazima wenye zaidi ya miaka 15 yanaendelea kupungua kutoka watu 72,000 waliokuwepo mwaka 2016/2017 hadi watu 60,000 kwa mwaka 2022/2023. Hii ni sawa upungufu wa asilimia 0.18 ambapo asilimia 0.24 ni wanawake na asilimia 0.11 ni wanaume.

Ikumbukwe kuwa Serikali iliamua kufanya utafiti kwa lengo la kujua hali ya sasa ya VVU na UKIMWI ilivyo hapa nchini na matokeo yameonesha kuwa Tanzania imepata mafanikio makubwa katika mapambano dhidi ya UKIMWI.

Utafiti huo unaotambulika kama Utafiti wa Viashiria vya UKIMWI kwa mwaka 2022/2023 unapima matokeo ya mwitikio wa Kitaifa wa UKIMWI nchini miongoni mwa watu wazima wenye umri wa kuanzia miaka 15 ukiwa na lengo la kukadiria kiwango cha maambukizi mapya ya VVU, ushamiri wa VVU, ufubazaji wa VVU kwa watu wanaoishi na VVU na utumiaji wa dawa kitaifa na kimikoa. 

SOMA PIA: https://gazetini.co.tz/2023/07/16/kill-challenge-inavyosukuma-jitihada-za-kudhibiti-ukimwi-nchini/

Utafiti huo umebaini kuwa kiwango cha kufubaza VVU kimeendelea kukua ambapo kwa sasa ni wastani wa asilimia 78 ambapo kwa upande wa wanawake kiwango kimekua kwa asilimia 80.9 na wanaume asilimia 72.2 ikilinganishwa na asilimia 52 iliyokuwepo kulingana na utafiti wa mwaka 2016/2017.

Kuhusu kiwango cha ushamiri wa VVU kwa umri kuanzia miaka 15 na zaidi kwa mikoa ya Tanzania bara, utafiti umeonesha kuwa, kinaanzia asilimia 1.7 kwa mkoa wa Kigoma hadi kufikia asilimia 12.7 kwa mikoa ya Njombe, Mbeya na Iringa.

Mkoa wa Njombe una viwango vya ushamiri zaidi ya asilimia 9 sawa na mara mbili ya kiwango cha Taifa. Kwa upande wa Zanzibar, yanaonesha unaanzia asilimia 0.2 katika Mkoa wa Kaskazini Pemba hadi asilimia 0.8 Mkoa wa Kusini Unguja.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img