1.4 C
New York

Visual|Maendeleo ya uokoaji wa waathirika Hanang

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Gazetini imekufanyia uchambuzi wa Taarifa fupi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyotolewa leo Desemba 5, 2023, kuhusu maendeleo ya kazi ya uokoaji wa waathirika na mali pamoja na utafutaji wa miili kufuatia janga la maporomoko ya tope, maji, mawe na magogo kutoka mlima Hanang mkoani Manyara.

Kwa ujumla kaya 1,150 zenye watu 5,600 zimepoteza makaazi yake katika mji mdogo wa Katesh na vitongoji vya Jorodom, Ganana, Katesh na Dumbeta pamoja na vijiji vya Gendabi, Sarijandu, Arukushay na Sebasi.

Aidha, pamoja na mambo mlengine, Serikali inatoa wito kwa kampuni, mashirika, taasisi za umma na binafsi, wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kujitolea kwa hali na mali ili kuwaisaidia wenzetu waliopatwa na janga hili. Bado tunahitaji vyakula, vifaa, mitambo, madawa na mahitaji mengine.

SOMA PIA: https://gazetini.co.tz/2023/12/04/waliofariki-katesh-wafikia-63-majeruhi-116/

Kwa misaada ya fedha, Waziri Mkuu ameelekeza, kwamba mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022 na kanuni zake za mwaka 2022, fedha zote zitumwe kwenye akaunti ya Kamati ya Maafa ya Taifa: National Disaster Management Fund Electronic Account 9921151001 kwa kuandika neno MAAFA HANANG. Benki yoyote ndani na nje ya nchi inaweza kupokea fedha kupitia akaunti hii.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img