1.4 C
New York

Visual| Ilichukua muda gani kwa idadi ya watu duniani kuongezeka kwa bilioni moja?

Published:

Na Jackline Jerome, Gazetini

Kwa mujibu wa Ripoti ya Makadirio ya Kati ya Umoja wa Mataifa(UN’s-Mid Year) Mwaka 2023 Dunia imefikisha watu bilioni 8. Idadi hiyo inafikiwia katika kipindi ambacho Tanzania imefikia watu milioni 61.74 kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika Oktoba 23, 2022.

Hiyo ni bayana kwamba idadi ya watu imekuwa ikiongezeka duniani kadri miaka inavyozidi kusonga, takwimu zinaonyesha kuwa dunia ilifikia watu bilioni moja mwaka 1805.

Marekebisho ya 2022 yamakadirio ya idadi ya watu kutoka Idara ya Umoja wa Mataifa ya Idadi ya Watu inaonyesha namna kasi ya uongezeko la watu inavyoongezeka duniani kadri muda unavyozidi kwenda.

Takwimu zinaonyesha kwamba kutoka mwaka 1805 ambapo dunia ilifikia watu bilioni 1, ilichukua miaka 120 baadae kufikia watu bilioni 2 ambayo hiyo ilikuwa mwaka 1925.

Safari ya kufikia watu bilioni 3 haikuwa ndefu ikilinganishwa na ile ya bilioni 2 kwani ilichukua miaka 35 kufikia idadi hiyo ambapo ilikuwa mwaka 1960. Hii ni sawa na kusema kwamba kiwango cha kuzaliana kiliongezeka duniani kwani miaka 14 baadae dunia ilikuwa na watu bilioni 4 ambapo ilikuwa mwaka 1974.

Miaka 13 baadae kwa maana wa mwaka 1987 dunia ilifikia watu bilioni 5 ikiwa. Mwaka 1999kwa maana ya miaka 12 baadae idadi ya watu duniani iliongezeka na kufikia bilioni 6, wastani huo uliendelea kwani miaka 12 baadae kwa maana ya 2011 dunia ilifikia watu bilioni 7.

Mwaka huu 2023 kwa maana ya miaka 12 tena baadae dunia imefikia watu bilioni 8 na hapa ndipo dunia ilipo hivi sasa katika idadi ya watu.

Hata hivyo, wataalamu wanatabiri kuwa idadi ya watu itaongezeka na kufikia bilioni 9 ifikapo mwaka 2037 kwa maana ya miaka 12 mingine baadae.

Ni matazamio ya wataalamu kwamba mwaka 2058 kwa maana ya miaka 21 baadae dunia itakuwa na watu bilioni 10.

Pia unaposoma andiko hili unapaswa kutambua kuwa makadirio ya hivi punde ya kati ya Umoja wa Mataifa yanatazamia kwamba dunia haitafikia watu bilioni 11 karne hii badala yake inakadiria idadi ya watu kufikia kilele bilioni 10.4 mwaka 2086.

Hii ni sawa nakusema kuwa idadi ya watu duniani inazidi kuongezeka kila iitwapo leo, hivyo ni wati wa Serikali na Watunga sera kuendelea kuja na mawazo na mikakati bora zaidi ambayo itasaidia kuifanya dunia kuendelea kuwa sehemu salama zaidi ya kuishi.

Kwani kwa miaka ya karibuni tunashuhudia namna ambavyo mabadiliko ya tabia nchi yanavyotishia ustawi wa dunia.

Athari hizo zikiwamo za mazingira siyo tu kwamba zimekuwa zikiathiri binadamu bali hata wanyama wamekuwa wakifa kwa kukosa chakula hali inayosababishwa na ukame na kukauka kwa mabwawa.

Idadi ya watu Afrika Mashariki kufikia mwaka 2050

Wakati takwimu za kidunia zikibainisha kuongezeka kwa idadi hiyo ya watu, wachambuzi wa masuala ya kimataifa wanaitazama Jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa kufikia mwaka 2050 itakuwa na jumla ya watu milioni 583.

Idadi hiyo inatokana kwamba, upande wa Kongo utakuwa na jumla ya watu milioni 195, ikifuatiwa na Tanzania watu milioni 129, Uganda milioni 100, Kenya milioni 92, Burundi milioni 25, Rwanda milioni 22 na Sudan Kusini milioni 20.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img