1.4 C
New York

Visual| Moto unavyotikisa uwepo wa Mlima Kilimanjaro

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Takwimu za Wizara ya Maliasili na Utalii nchini zinachambua kuwa Sekta ya Utalii inachangia asilimia 17.5 ya Pato la Taifa huku ikiipatia nchi asilimia 25 ya fedha zote za kigeni.

Kama hiyo haitoshi sekta hiyo inatoa ajira za moja kwa moja 600,000 na nyinginezo zaidi ya 2,000,000. Ikumbumbe kuwa ndani sekta hiyo kuna Idara ya Mambo ya Kale na hifadhi za taifa zilizo chini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Na unapozigusa hifadhi za taifa 22 zilizopo nchini, kuna Hifadhi ya Taifa Serengeti na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) ambazo kimapato zinasaidia kuendesha hifadhi zingine za taifa zenye mapato kidogo.

Hata hivyo, wakati sekta hiyo ikiendelea kuwa tegemeo kwa kuingiza fedha za kigeni na kuchangia Pato la Taifa, uendelevu wa ikolojia na utalii wa KINAPA uko shakani kutokana na matukio ya moto yanayoikumba hifadhi hiyo mara kwa mara.

Itakumbulkwa tukio la hivi karibuni ni la usiku wa Oktoba 21 mwaka huu, moto ulipozuka kwenye Kambi ya Karanga na kuteketeza uoto wa asili kwenye eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 34, kwa mujibu wa Ofisa Uhifadhi Mwandamizi -Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Catherine Mbena.

Kambi hiyo iko umbali wa mita 3,963 kutoka usawa wa bahari, eneo hilo likiwa na sifa ya kuwa na mimea aina ya Erica na Protea, inayoshika moto kwa kasi wakati wa ukame. Aidha, kanzidata ya KINAPA, ina matukio mengine makubwa manne ya moto kwenye eneo hilo la hifadhi yaliyotokea ndani ya miaka mitano kuanzia 2015/16.

Kanzidata hiyo inaonesha kuwa mwaka 2015/16 eneo lililoteketea kwa moto ni hekta 49.13, mwaka 2016/17 hekta 17, mwaka 2017/18 hekta 82, mwaka 2018/19 hekta 72.3 na la Oktoba 2020 hekta 22.05, kiini kikuu kikitajwa kuwa uvunaji mbaya wa asali, ujangili na mbinu mbaya za kilimo.  

Zaidi www.gazetini.co.tz imekuchambua hali halisi ya hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ambao ni kivutio cha watalii Barani Afrika, kwa kutumia usanifu hapo juu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img