22.9 C
New York

Chart| Waandishi wa Habari waliofungwa gerezani kutokana na kazi yao

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Mei 3 ya kila mwaka huazimishwa Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, ni tukio muhimu lkwa ajili ya kusherehekea kanuni za msingi za uhuru wa vyombo vya habari, kutathmini hali ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kote na kutetea haki za waandishi wa habari.

Sambamba na hayo, siku hii hutumika kuangalia umuhimu mkubwa wa vyombo vya habari huria katika jamii za kidemokrasia. Kwani kama inavyofahamika kuwa uhuru wa vyombo vya habari ni nguzo ya msingi ya demokrasia.

Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ilitangazwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 1993, kufuatia pendekezo lililopitishwa katika kikao cha ishirini na sita cha Mkutano Mkuu wa UNESCO mwaka 1991. Inatumika kama ukumbusho wa jukumu muhimu ambalo vyombo vya habari huru hutimiza jukumu lake katika kukuza demokrasia na kukuza haki za binadamu.

Uhuru wa Vyombo vya Habari unalinda haki ya umma ya kupata habari mbalimbali na kuwawajibisha walio madarakani. Kudumisha uhuru wa vyombo vya habari ni muhimu kwa kukuza uwazi, kukuza ufanyaji maamuzi sahihi na kulinda kanuni za kidemokrasia duniani kote.

Hata hivyo katika #CHART yetu tumeangazia Waandishi wa Habari waliofungwa gerezani duniani kote kwa kiwango cha juukutokana tu na kazi yao.

Takwimu hizo zilizotolewa na Kamati ya Kulinda Waandishi wa Habari duniani(CPJ) zinaonyesha kuwa mwaka 2022 kulikuwa na kiwango cha juu cha waandishi wa habari waliofungwa gerezani duniani kote kuhusiana na taaluma yao.

Kulingana na takwimu hizo kiwango cha waandishi wa habari waliofungwa gerezani kilikuwa karibu mara mbili mwaka 2022 ambapo jumla ya waandishi 363 walifungwa gerezani duniani kote kutokana na kazi yao ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo walikuwa waandishi wa habari 198.

Zaidi angalia chart yetu kuona mwenendo wa matukio hayo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img