1.4 C
New York

Chart| Madhila yaliyowapata Waandishi wa Habari nchini Tanzania Mwaka 2023

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

MATUKIO ya wanahabari kunyimwa taarifa kwenye vyanzo vya habari yameripotiwa kuwa mengi zaidi ukilinganisha na yale ya vitisho, kukamatwa, kupigwa, kufungiwa, kuingiliwa kwa uhuru wa uhariri, kutozwa faini.

Kwa mujibu Ripoti iliyotolewa mapema mwaka huu na Afisa Program Baraza la Habari Tanzania (MCT), Paul Mallimbo, inaonyesha kuwa hadi kufikia Desemba
2023 yamerekodi madhira 27 kwa waandishi wa habari nchini Tanzania.

Kati ya hayo, matukio  ya kunyimwa taarifa yalikuwa saba, vitisho matano, kukamatwa matano, kupigwa mawili, kufungiwa vyombo vya habari mawili, kuingiliwa kwa uhuru wa uhariri moja, kutozwa faini moja, kipindi kukatishwa moja na kushambuliwa.

Aidha, matukio hayo yaliwakumba waandishi wa habari 27 ambapo kati yao wanaume ni 18 na wanawake  wanane.

“Idadi hiyo ni ongezeko la waandishi wa habari wanane ambao walikumbwa na madhira mwaka 2022 ambapo walikuwa 19, kati yao wanaume 10 na wanawake tisa,” amebainisha Mallimbo.

Aliongeza kuwa mikoa ambayo waandishi waliripotiwa kupata madhila ni pamoja na Dar es Salaam tisa, Mara mmoja, Shinyanga watatu, Kilimanjaro wawili, Mwanza mmoja, Mbeya wanne, Dodoma watatu, Njombe mmoja, Morogoro wawili na Unguja mmoja.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img