22.9 C
New York

TACAIDS yakutana na Wadau kupitia rasimu tatu za uratibu wa afua za vijana balehe nchini

Published:

Na Nadhifa Omary, TACAIDS

Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania kwa kushirikiana na wadau wamekutana kupitia, kujadili na kuthibitisha rasimu tatu za uratibu wa afua za Vijana Balehe nchini.

Rasimu hizi ni mfumo wa pamoja wa  ufuatiliaji na tathimini shughuli za vijana balehe katika Mwitikio wa UKIMWI, Mpangilio wa Afua za Vijana Balehe SOP na Kanzi data ya kuhifadhi afua za vijana balehe ambazo zinatekelezwa na wadau wa UKIMWI hapa nchini.

Baadhi ya wadau wanaotekeleza afua za UKIMWI ambazo zinawalenga vijana balehe wakiendelea na zoezi la kupitia rasimu zinazopendekezwa kutumika katika uratibu wa afua za UKIMWI kwa vijana Balehe.  kikao hiki kilichofanyika jijini Dodoma Februari  8 na 9, 2024.

Baadhi ya wadau wakipitia mapendekezo ya rasimu zinazopendekezwa kwa ajili ya uratibu wa afua za UKIMWI ambazo zinawalenga vijana na kutoa maoni kwa lengo la kuboresha na kuhakikisha rasimu hizi zinazingatia mahitaji ya wapokea huduma na watoa huduma.
Dk. Julius Sipemba kutoka shirika la THPS. akiwasilisha maoni yaliyotolewa na moja ya kundi ambalo lilishiriki kwa ajili ya kupitia Mpangilio wa Afua za Vijana Balehe SOP lengo ikiwa ni kuhakikisha nyenzo hiyo inakuwa na maoni ya wadau wote.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img