1.4 C
New York

Infographic| Tunachofahamu SIKU 74 za mzozo wa Israel-Gaza

Published:

Na Faraja Masinde, Gazetini

-Kwa msaada wa mashirika mbalimbali ya habari

Takriban watu 21,107 wameuwa wakiwamo watoto 7,802 wa Palestina tangu kuanza kwa mashambulizi ya Isarael na Palestina Oktoba 7, mwaka huu.

Kulingana na Takwimu za hadi leo Desemba 19, 2023 saa 7:00 mchana zinaonyesha kuwa katika mchanganuo huo watu 19,667 wameuawa upande wa Gaza-Palestina wakiwamo watoto 7,729 kutokana na mashambulizi hayo.

Upande wa Israel idadi rasmi ya waliouawa kutokana na mashambulizi ya Hamas inafikia zaidi ya 1,139 wakiwamo Watanzania wawili Joshua Mollel(21) na Clelemence Mtenga(22) ambao walikuwa masomoni nchini humo.

Aidha, takriban watu 301, wakiwemo watoto 72, wakiuawa katika Ukingo wa Magharibi(Occupied West Bank).

Kando ya waliopoteza maisha, watu wengine 64,681 wamejeruhiwa vibaya wakiwamo watoto 8,663 wa Palestina.

Aidha, majengo 40,000 sawa asilimia 18 ya majengo yote ya kabla ua kuanza kwa mapigano hayo yameharibiwa katika ukanda wa Gaza.

Umoja wa Mataifa(UN) umebainisha kuwa asilimia 85 ya Wapalestina wameyakimbia makazi yao.

Wito wa kusitishwa kwa mapigano

Viongozi mbalimbali duniani wameendelea kushinikiza juu ya kusitishwa kwa mgogoro huo ambao leo Desemba 19 umefikisha siku ya 74 tangu ulipoanza Oktoba 7, mwaka huu.

Kabla ya kura ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa inayotarajiwa baadaye leo kuhusu azimio jipya la kusitisha mapigano Gaza, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Kibinadamu, Volker Turk, amewataka wanachama wa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono usitishaji vita hiyo endelevu katika eneo hilo.

Anasema wito wa kusitisha mapigano kwa misingi ya haki za binadamu na kibinadamu “unazidi kuongezeka siku hadi siku, na lazima uzingatiwe,” amesema Turk huku akikiri kwamba makumi ya maelfu ya watu ni wakimbizi wa ndani katika Ukanda huo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img