3.2 C
New York

Visual| Serikali yaendelea kupokea misaada Hanang

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Serikali imeendelea kupokea misaada mbalimbali kutoka kwenye taasisi za umma na binafsi likiwemo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Umoja wa Watoa Huduma za Mawasiliano ya Simu Tanzania (TAMNOA)
pamoja na klabu mbili za mpira wa miguu nchini za Simba na Yanga.

Serikali inatoa wito kwamba wananchi na wadau mbalimbali wa ndani na nje kuendelea kutoa misaada yao hali na mali.

Kamati ya Maafa ya Taifa iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022 imetoa Electronic Account iitwayo National Relief Fund – Na. 9921159801– ambamo miamala inaweza kutumwa kwa utambuzi wa maneno MAAFA HANANG. Akaunti hiyo ipo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na inapokea fedha kutoka ndani na nje ya nchi.

Leo Desemba 6, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano yuko ziarani hapa Katesh kuangalia madhara yaliyotokea, kukagua huduma za uokoaji na misaada inayotolewa, kuwatembelea waathirika waliolazwa hospitalini pamoja na waliopo kwenye kambi na kuwapa pole wananchi wa Hanang.

Kesho Alhamisi Desemba 7, 2023, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dk. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kufanya ziara hapa Katesh kwa lengo hilo hilo la kuwapa pole wananchi na kutoa maelekezo mengine ya kazi inayoendelea hapa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img