1.4 C
New York

Dk. Yonazi aridhishwa na maandalizi ya Kuelekea Siku ya UKIMWI Duniani

Published:

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dk. Jim Yonazi ametembelea mabanda mbalimbali na kujionea maandalizi yaliofanywa na wadau mbalimbali kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yatakayofanyika Desemba Mosi,2023 katika Viwanja vya Morogoro Sekondari ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa.

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Jamii Iongoze Kutokomeza UKIMWI”

Aidha, ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wananchi kujitokeza katika maadhimisho hayo na kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI nchini.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img