21 C
New York

Kipengele cha Gesi, Mafuta na Madini charudishwa tuzo za EJAT

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Kamati ya Maandalizi ya Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) 2023, imelirudisha kundi la Habari za Gesi, Mafuta na Uchimbaji Madini kuanzia Novemba 19, 2023.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Kajubi Mukajanga amesema hatua hiyo inafuatia maombi mengi yaliyowasilishwa kwake yakitaka kundi hilo liwe miongoni mwa makundi yanayoshindaniwa katika Tuzo za mwaka huu.

Kajubi anawaomba waandishi kulitangaza kundi hilo, ili lipate ufadhili na kazi nyingi zenye umahiri kutoka kwa waandishi wa habari. Kufuatia hatua hiyo, idadi ya makundi yatakayoshindaniwa itakuwa 19 badala ya 18.

SOMA PIA: https://gazetini.co.tz/2023/11/15/tuzo-za-ejat-2023-zazinduliwa-dodoma/

Itakumbukwa, Novemba 15, mwaka huu akizungumza wakati wa uzinduzi wa tuzo hizo kwa mwaka 2023 uliofanyika jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya EJAT, Kajubi Mukajanga alisema; “Pamoja na nyongeza ya makundi hayo, makundi ya Habari za Gesi, Mafuta na Uchimbaji Madini, Habari za Sayansi na Teknolojia; na Habari za Sensa yameondolewa katika orodha ya makundi yatakayoshindaniwa katika Tuzo hizo.

“Hii ni kutokana na mwitikio mdogo wa uwasilishaji kazi kutoka kwa waandishi wa habari na kukosekana kwa ufadhili wa uhakika,” alisema Mukajanga.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img