7.8 C
New York

Fahamu| Manyara yaongoza kwa kuwa na wanaume wengi

Published:

Na Mwandish Wetu, Gazetini

Kulingana na Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yaliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu(NBS), Manyara ndiyo Mkoa pekee wenye idadi kubwa ya wanaume kuliko wanawake Tanzania.

Kwa mujibu wa NBS, mkoa huo wenye jumla ya wakazi 1,892,502 kati yao wanaume ni 954,879 huku wanawake wakiwa 937,623.

Hii ni sawa na kusema kwamba kuna wanaume 17,256 zaidi ikilinganishwa na wanawake.

Aidha, katika mikoa mingine ya Tanzania iliyosalia matokeo hayo yanaonyesha kuwa wanawake ni wengi kuliko wanaume.

Je, unafikiri hii imesababishwa na nini kwa mkoa huu wa Manyara? tuandikie kwenye comment.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img