1.7 C
New York

Visual| Kituo cha Maarifa Manyoni kinavyosaidia mapambano ya VVU

Published:

*Kamati ya Bunge ya Afya na UKIMWI yapongeza

Na Nadhifa Omar, Singida

Kituo cha Maarifa cha Manyoni mkoani Singida kimechangia katika mikakati ya Taifa ya utoaji elimu ya kupunguza ongezeko la maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI(VVU), kutokana na kujengwa kando kando ya barabara yanapoegeshwa magari ya masafa marefu ikiwa ni hatua ya inayoelenga kufikia makundi yaliyo katika uhatarishi wa kupata  maambukizi ya mapya ya VVU.

Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga akizungumza na wananchi na wakazi wa halimashauri ya Manyoni wanaopata huduma katika kituo cha maarifa Manyoni mara baada ya kutembelea kituo hicho alipokuwa ameambatana na kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Msuala ya UKIMWI Oktoba 10, 2023 kwa lengo la kutembelea shughuli zinazotekelezwa na TACAIDS.

Hayo yamejiri Oktoba 10, 2023 wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI ilipotembelea kituo cha maarifa cha Manyoni mkoani Singida na kujionea shughuli zinazotekelezwa katika kituo hicho.

Akiwasilisha taarifa ya kituo hicho mbele ya kamati hiyo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manyoni Dk. Furaha Mwakafwila amesema  kituo hicho kilijengwa mwaka 2016 na  Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS) kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu Geita Gold Mining(GGML) ikiwa ni moja ya jitihada za serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi katika kupambana na maambukizi mapya ya VVU.

“Kituo hiki kilijengwa mwaka 2016 na TACAIDS kwa kushirikiana na GGML ambapo kiligharimu jumla ya Shilingi 87,584,077. Lengo ikiwa ni ni kutoa huduma kwa madereva wa masafa marefu, wasafiri wanaotumia barabara kuu Dar es Salaam, Tabora na Singida pamoja na watu wote wanaoishi Manyoni,” amesema Dk. Furaha.

Aidha, ametoa taarifa ya huduma ya upimaji wa VVU katika kituo hicho kuanzia mwaka 2022 hadi 2023 jumla ya watu 1,990 wamepima afya zao, ambapo wanaume ni 983 na wanawake ni 1,007, madereva ni 684.

Jumla ya watu 19 waligundulika kuwa na maambukizi ya VVU ikiwa ni pamoja na kuunganishwa katika kliniki za Tiba na Matunzo.

Ameipongeza Serikali kwa wazo la kushirikisha wadau na kuona umuhimu wa kujenga kutuo hicho katika halmashauri ya Manyoni ili upimaji wa VVU, kondomu pamoja na kupata ARV kwa wale ambao tayari wamepima kuanza dawa waweze kuchukua dawa iwapo itatokea mtu kaishiwa akiwa safarini hasa kwa madereva wa masafa marefu, wasafiri wanaotumia barabara kuu ya Dar es Salaam, Tabora na Singida pamoja na watu wote wanaoishi Manyoni.

Ameongeza kuwa anashukuru kituo hiki kuongezewa huduma za zahanati kwani zimepelekea kituo hiki kuimarika zaidi na kuendelea kukuwa kwani sasa wananchi wanaozunguka katika eneo hilo ndio imekuwa zahanati yao kuu ya kupata huduma zote, kwakuwa awali ilikuwa ni kwa ajili ya huduma za HIV tu tofauti na sasa.

Dk. Furaha amewataka wakazi wa Manyoni kukitumia kituo hicho katika kupata huduma kwani zipo na watoa huduma wapo.

“Wananchi wasihangaike kwenda mbali kwa ajili ya kutafuta huduma za Afya,”

Dk. Furaha.

“Wananchi wasihangaike kwenda mbali kwa ajili ya kutafuta huduma za Afya,” amesema Dk. Furaha.

Alibainisha baadhi ya mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa kituoni hapo kuwa ni pamoja na kituo kusajiliwa kutoa kutoa huduma za NHIF na CHIF, kuongezeka kwa idadi ya wateja hasa akina mama katika kliniki ya huduma za mama na mtoto.

Dk. Ainea Mlewa Mratibu wa UKIMWI –Afya Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida akifafanua namna wanavyotekeleza majukumu yao kituoni hapo wakati wa ziara ya Kamati ya kudumu ya Bunge ya Afya na Msuala ya UKIMWI, wanaomsikiliza ni baadhi ya wabunge wa kamati hiyo, na aliyekaa amevaa sare nyeupe ni Muhudumu wa Afya Kituo cha Maarifa Manyoni, Getrude Sebastian.

Pia, kuongezeka kwa wateja wanaokuja kupata huduma za ushauri nasaha na kupima afya zao, kupata kisima chenye maji mengi ambayo yamekuwa msaada kwa kituo hicho pamoja na wakazi wa jirani, kiuto kusajiliwa kutoa huduma ya Tiba na matunzo (CTC).

Kuwepo kwa kamati ya maborshao na matunzo pamoja na kuundawa kwa vikundi vya utoaji Elimu kwa jamii.

Upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Ummy Nderiananga amewapongeza watendaji wa kituo hicho kwa kazi nzuri wanaoitaka na kuwataka wananchi wa halmashauri ya Manyoni kuto sita kutembelea kituo hicho ili kupata huduma zinazotolewa.

Pamoja na ziara hiyo baadhi ya wabunge walishiriki kupima VVU na kendelea kuhamasisha umma, wa kila mmoja kujua afya yake.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img