21 C
New York

Visualization| Miaka 60 ya Uchumi Tanzania

Published:

KAMA inavyofahamika kwamba Desemba 9, kila mwaka, ni kumbukizi ya uhuru wa Tanzania kutoka kwa Waingereza na kwa mwaka huu itakuwa ni miaka 60 tangu ilipojitoa kwenye minyororo ya Wakoloni hao.

Maandalizi ya kuelekea kwenye kilele cha Siku ya Uhuru yanaendelea, ikiwa ni pamoja na Serikali kupitia wizara zake kuendelea kuainisha mafanikio yaliyopatikana hadi sasa katika nyanja tofauti tofauti.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba ameingia kwenye orodha ya mawaziri waliokwisha bainisha changamoto na mafanikio yaliyopatikana tokea nchi ilipopata uhuru Desemba 9, 1961.

Kwa mujibu wa Dk. Nchemba ndani ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, kiwango cha umaskini kimepungua kutokana na jitihada za serikali katika kuboresha huduma za msingi za jamii ikiwemo upatikanaji wa maji, umeme, huduma za afya, utoaji wa elimu msingi bila malipo.

Amesema kiwango cha umaskini na mahitaji ya msingi kimepungua hadi asilimia 25.7 mwaka 2020 kutoka asilimia 38.6 mwaka 1992.

Pia amesema takwimu zinaonesha kuwa ukuaji wa uchumi katika kipindi cha miaka 60  ya uhuru ulikuwa ukipanda na kushuka kutokana na sababu mbalimbali lakini haujawahi kufikia ukuaji hasi huku akidai Nchi inajivunia kuingia uchumi wa kati.

Akizungumza Novemba 11,2021, kuhusu maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara, Waziri Nchemba amesema tangu uhuru, uchumi wa Tanzania umepitia katika nyakati mbalimbali za mafanikio ya kiuchumi pamoja na changamoto kadhaa.

Ameziataja changamoto hizo kuwa ni pamoja na ukame katika miaka ya mwanzoni mwa 1970 na 2012, mdororo wa uchumi wa mwaka 2008, vita vya Kagera mwaka 1978 pamoja na ugonjwa wa UVIKO mwaka 2020.

Hata hivyo, Serikali kupitia mikakati mbalimbali iliweza kujikwamua kutokana na magumu hayo iliyopitia na hii iliwezesha katika historia ya Tanzania kutokuwa na ukuaji hasi wa uchumi  tangu uhuru.

Amesema takwimu zinaonesha kuwa ukuaji wa uchumi katika kipindi cha miaka sitini ya uhuru ulikuwa ukipanda na kushuka kutokana na sababu mbalimbali lakini haujawahi kufikia ukuaji hasi.

Amesema wastani wa ukuaji wa uchumi katika kipindi cha Serikali ya awamu ya kwanza (1967 – 1985) iliyoongozwa na mwasisi na Baba wa Taifa  Hayati Mwalim Juluis Kambarage Nyerere ulikuwa asilimia 3.1; Serikali ya awamu ya pili (1986 – 1995) asilimia 3.0, Serikali ya awamu ya tatu (1996 – 2005) asilimia 5.7, Serikali ya awamu ya nne (2006 – 2015) asilimia 6.3, na Serikali ya awamu ya tano (2016 – 2020) asilimia 6.5.

PATO LA TAIFA

Waziri huyo wa Fedha na Mipango amesema Pato la Taifa lilikua kwa asilimia 4.8 ikilinganishwa na asilimia 7.0 mwaka 2019 ambapo amedai sababu kuu ya kupungua kwa kasi ya ukuaji ni athari za hatua zilizochukuliwa na mataifa mbalimbali duniani ambao ni washirika wakubwa wa biashara wa Tanzania katika kukabiliana na janga la UVIKO-19.

“Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na mataifa hayo ni pamoja na kufunga mipaka, kusitisha safari za ndege za kimataifa na kusitisha baadhi ya shughuli za kiuchumi zinazohusisha mikusanyiko,”amesema waziri huyo.

Amesema hatua hizo zilisababisha uchumi wa dunia kuporomoka mwaka 2020 ambapo nchi nyingi zilikuwa na ukuaji hasi na kwa nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, ni nchi 11 tu zilikuwa na ukuaji chanya kati ya nchi 45.

Zaidi angalia Usanifu wetu hapo juu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img