1.7 C
New York

Chati| Soko la nje linavyoitajirisha Tanzania

Published:

KATIKA dhana nzima ya utandawazi, haiepukiki kutaja fursa lukuki za kiuchumi zinazotokana na ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi moja na nyingine. Ni kwa ushirikiano huo, nchi moja na nyingine hujikuta zikinufaishana kwa fedha za kigeni.

Aidha, si tu kwa taifa, bali pia ushirikiano wa kibiashara huwezesha wananchi (wakulima na wafanyabiashara) kutanua wigo wao kiuchumi, achilia mbali uhakika wa soko la bidhaa zao.

Kwa Tanzania, kama zilivyo nchi zingine zinazoendelea, nayo imekuwa ikinufaika na uzalishaji na usafirishaji wa bidhaa zake kwenda nchi mbalimbali.

Takwimu zinaonesha kuwa kuanzia mwaka 2016-20, Tanzania imevuna fedha nyingi za usafirishaji wa bidhaa zake nje ya nchi. Kwamba jumla ya Sh bil. 5,254.1 zilipatikana kwa mwaka 2016 kutokana na usafirishaji wa kahawa, pamba, katani, korosho, karafuu, almasi, dhahabu, tumbaku, na chai.

Kati ya bidhaa hizo, dhababu na kahawa zimeonekana kuwa kwenye kiwango cha juu zaidi. Mathalan, kwa mwaka 2016 pekee, madini hayo yaliingiza kwenye pato la Taifa kiasi cha Tsh bil. 3072.7. Mwaka huo, tumbaku ilishika nafasi ya pili baada ya kuingiza Tsh bil. 783.

Mazao mengine na kiasi cha fedha kilichopatikana kwa mwaka huo yameanishwa vizuri kwenye chati yetu. Mwaka uliofuata, 2017, Tanzania iliendelea kuvuna fedha za kigeni, ikiingiza Tsh bil. 5,847.5 kwa bidhaa zake zilizokwenda nje.

Mwenendo wa bidhaa zilizouzwa nje 2016-2020 (Tsh Bilioni)

Bidhaa20162017201820192020
Kahawa224.2282.4337.5351.0331.5
Pamba100.580.3157.2212.0199.8
Katani32.357.746.953.840.1
Korosho756.91200.5287.9821.9824.6
Karafuu22.5121.20.720.838.9
Almasi164.3143.0184.2185.046.1
Dhahabu3072.73418.93435.75043.16752.4
Tumbaku783.8434.5609.7389.5339.4
Chai96.9109.0103.3104.073.9

Kama kawaida, dhahabu ilikuwa kinara kwa mara nyingine (Sh bil. 3418.9), ikifuatiwa na korosho (Tsh bil. 1200.5). Chati yetu inafafanua zaidi juu ya mazao mengine yaliyosafirishwa kwa mwaka huo.

Aidha, wakati Tanzania ikipata Tsh bil. 5,163.1, usafirishaji wa dhahabu ulichanua tena mwaka 2018, ambapo nchi iliingiza Tsh bil. 3,435, nafasi ya pili ikishikwa na tumbaku iliyoingiza kwenye pato la Taifa kiasi cha Tsh bil. 609.7.

Chati yetu haijasahau kuanika takwimu za mazao mengine. Tanzania ilinufaika tena mwaka 2019 kwa bidhaa zake zilizosafirishwa kuingiza tsh bil. 7,181.1. Vilevile, madini ya dhahabu yalishika nafasi ya kwanza (Tsh bil. 5,043.1), yakifuatiwa na korosho (Tsh bil. 821).

Mwaka jana, 2020, ilikuwa ni neema pia kwa Tanzania kwenye usafirishaji wa bidhaa zake nje ya nchi. Fedha za kigeni zilizoingia zilifikia Tsh bil 8,646.7.

Kama ilivyokuwa mwaka 2019, dhahabu iliongoza (Tsh bil. 6,752) na kisha korosho ikashika nafasi ya pili (Tsh bil. 824.6).

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img