14.4 C
New York

Msanii Chemical apongezwa kufaulu mtihani wa PhD, rasmi ni Dk Lubao

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Mashabiki wa msanii wa muziki wa hip-hop Tanzania, Claudia Lubao maarufu Chemical, wamempongeza msanii huyo kwa kufanikiwa kufaulu mtihani wake wa mwisho wa shahada ya uzamivu (PhD) ambapo rasmi anaitwa Dk Lubao.

Chemical amehitimu shahada hiyo katika Chuo Kikuu cha St Andrew, Uingereza. Kupitia mitandao yake ya kijamii, Chemical ametoa ujumbe wa shukrani uliogusa watu wengi na kuanza kumimina pongezi kwake.

Katika ujumbe huo amesema: “Nilikuwa na ndoto, na leo nimeamka kama Dk Lubao!”

Kabla ya kwenda huko kwa ufadhili wa kimasomo alifanya vizuri pia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alikosoma shahada ya kwanza ya sanaa za maonesho, baadaye shahada ya uzamili katika usimamizi wa urithi wa kitamaduni.

Ametoa pongezi kwa wasimamizi, idara mbalimbali, jopo la watahini, marafiki, na mashabiki waliompa moyo katika safari hiyo ya kitaaluma.

Shahada yake ya uzamivu inahusiana na urithi wa kitamaduni na mchango wa muziki wa kizazi kipya katika kuwasilisha masuala ya kijamii kama mabadiliko ya tabianchi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img