20.4 C
New York

Infographic| Ufanisi wa TIC kwa miaka mitatu

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

TANZANIA ni miongoni mwa nchi zenye fursa nyingi za uwekezaji katika Ukanda huu wa Afrika Mashariki, sambamba na hilo kwa siku za karibuni imekuwa kivutio kikubwa kwa wawekezaji kutokana na kuwapo kwa sera na mazingira mazuri yanayochangiza uwekezaji huo.

Mageuzi hayo makubw aya kisera yamefanyika chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

Itakumbukwa Mei 5, 2021 akiwa ziarani nchini Kenya, Dk. Samia alisema kuwa lengo lake ni kuhakikisha kwamba wawekezaji wa kigni wanajenga imani ya kuwekeza nchini Tanzania na ili kurahisisha hilo Serikali imeanzisha miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo ya miundombinu kama barabara, reli, bandari ili kupunguza gharama ya kufanya biashara.

Julai 17, mwaka huu akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JINCC) jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC), Gilead Teri, alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kukaribisha wawekezaji na kuweka mazingira rafiki ili kuwavutia zaidi katika nyanja mbalimbali jambo litakalochangia kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Teri, uwekezaji ni nyenzo muhimu kwa ukuaji wa uchumi nchini kwa maendeleo ya sasa na vizazi vijavyo na kwamba jukumu lao ni kuhakikisha kuwa wawekezaji wanaongezeka kwa ajili ya kufungua fursa zaidi.

Kulingana na Teri, TIC ina mpango wa kuvutia uwekezaji wa dola bilioni 2 za kimarekani ndani ya miaka mitatu ijayo ikiwa ni pamoja na sekta za kawaida na mpya.

“Majukumu ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania ni pamoja na kuwafikia na kutoa chachu ya uwekezaji kwa wawekezaji wazawa na wageni, kuvutia uwekezaji kwenye fursa za uwekezaji nchini na kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji, ongezeko la watanzania katika miradi ambayo tunaisajili katika Kituo cha Uwekezaji ni kubwa.

“Hivyo, kuna muamko wa Watanzania kuingia ubia, kuna muamko wa Watanzania kusajili miradi mipya lakini pia kuna ongezeko na muamko mkubwa wa miradi ya wawekezaji kutoka nje,” amebainisha Teri na kuongeza kuwa kwa kipindi cha kuanzia January 2021 mpaka Juni mwaka huu TIC imesajili jumla ya miradi ya uwekezaji na maendeleo 778, ambapo inatajwa kuwa imesaidia kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kwa kutengeneza zaidi ya ajira mpya 125,382.

“Thamani ya miradi hiyo ni dola za kimarekani milioni 10,532, Serikali imeongeza wigo wa mapato kwa miradi hiyo kusajaliwa, lakini pia miradi hiyo imeleta teknolojia mpya kutoka mataifa mengine,” amesema Teri.

Teri amesema kuwa kituo hicho kitaendelea kuwasaidia wawekezaji baada ya kuwekeza ili wasipate changamoto za aina yoyote kupitia huduma kwa wateja, ambapo kwa sasa Kituo hicho kimeanzisha utaratibu wa kukutana na sekta mbalimbali pamoja na wawekezaji ili kujua changamoto ambazo wanazo na kwa namna gani wanaweza kuishauri Serikali namna ya kuboresha mazingira ya uwekezaji.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img