8 C
New York

Infographic| Maambukizi mapya ya VVU bado ni mtego kwa vijana

Published:

*TACAIDS yasema mapambano bado hayajaisha

*Nyenzo ya Kondomu yasisitizwa

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Maambukizi mapya ya Virusi Vya UKIMWI ni kama bado yameendelea kuwa mtego kwa vijana kutokana na takwimu kutkulibeba kundi hilo muhimu katika kuijenga Tanzania ijayo.

Mathalani takwimu za mwaka 2021 zilizotolewa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania(TACAIDS) zinaonyesha kuwa maambukizi mapya kwa nchini ni watu 54,000 katika maambukizi hayo asilimia 62.2 ni ni wanawake huku vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24 wakichangia asilimia 28 ya maambukizi hayo.

Aidha, takwimu hizo zinaenda mbali zaidi kwa kuweka wazi kuwa katika kiwango hicho cha vijana asilimia 73 ya maambukizi mapya kwa vijana yanatokea kwa wasichana.

Hii ni sawa na kusema kwamba vijana hususan wasichana bado wanachochea kwa sehemu kubwa katika maambukizi ya VVU.

Ikumbukwe kuwa kwa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika Oktoba 23, 2022 yanaonyesha kuwa kundi la vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 29 nchini Tanzania ni 16,576,537 ambapo kati yao wavulana ni 7,877,947 huku wasichana wakiwa 8,698,590.

Hii ni sawa na kusema kwamba kundi hilo pekee ni asilimia 21.17 ya Watanzania wote milioni 61,741,120. Hivyo basi kuna kazi ya kufanya katika kuhakikisha kwamba nyenzo hiyo muhimu katika ujenzi wa Tanzania ijayo inabaki salama pasi kuwa na maambukizi ya VVU.

Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Leonard Maboko anasema kuwa moja ya hatua za Serikali nikushirikisha Sekta Binafsi katika kudhibiti maambukizi ya VVU huku akisisitiza kuwa mapambano bado hayajaisha.

“Mapambano ya VVU bado hatujafikia mwisho, malengo ya kidunia ni kuwa ifikapo 2030 tuwe tumefikia Sifuri tatu kwa maana kuwa tuwe tumemaliza maambukizi mapya, tuwe tumemaliza unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU na familia zao na tuwe tumemeliza vifo vitokanavyo na UKIMWI.

“Kwa upande huo inatia moyo kutokana na kuwa miaka10 iliyopita, mwaka 2010 maambukizi mapya yalikuwa 110,000 kwa mwaka. Kwa takwimu za mwaka 2021 maambukizi mapya ni 54,000 hizi ni takwimu kwa mujibu wa makadirio ya mwaka 2021. Taarifa ya utaifiti mpya wa mwaka 2022/23 umeishaanza na upo katika hatua za mwisho utatolewa ndani ya miezi miwili hadi mitatu ijayo,” amesema Dk. Maboko.

Aidha, Dk. Maboko anasema kuwa katika lengo la kumaliza vifo mwaka 2010 kulikuwa na vifo vinavyotokana na UKIMWI 35,000, lakini kwa makadirio ya mwaka 2021 ni watu 29,000 na kwamba katika maeneo hayo mawili kama nchi imeshapunguza kwa asilimia 50.

“Kwa upande wa unyanyapaa kwa takwimu za mwaka 2013 zilikuwa ni asilimia 28 na kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka 2021 unyanyapaa umefika asilimia 5.5. Kwa takwimu hizi bado lengo bado halijafikiwa kwa kuwa lengo ni miaka saba ijayo malengo yote yawe yamefikia sifuri.

“Kwa maana hiyo kwa kadri wafadhili wanavyopunguza fedha tunatakiwa kuweka mkazo sana Watanzania wenyewe, kampuni zetu pamoja na wafanyabiashara ndani ya nchi yetu wote tuchangie katika mapambano dhidi ya VVU. Nawahamasisha waalikwa wote tuitikie na kupokea kuwa suala la UKIMWI ni la kila mmoja wetu kwani hakuna Mtanzaia ambaye hajawahi kupata athari za UKIMWI katika maisha yake.

“Pia ni muhimu kulida nguvu kazi katika maeneo yetu ya kazi ili tuweze kutoa maambukizi mapya kwenye 54,000 hadi maambukizi sifuri bado ni kazi kubwa ya kufanya,” anasema Dk. Maboko.

Kuhusu kumalizika kwa vifo vitokanavyo na UKIMWI anasema kuwa bado kuna kusuasua sana kwenye kupima ambapo kwa mujibu wa takwimu ni takribani watu 1,700,000 wanakadiriwa kuishi na VVU nchini lakini walipo kwenye dawa ni watu 1,500,000 tu.

“Kwa hiyo watu 200,000 siyo kazi rahisi, hivyo ushirikiano wa pamoja kwa Watanzania unahitajika ili tufikie malengo ya kidunia ya kumaliza UKIMWI ifikapo 2030,” anssema Dk. Maboko.

Matumizi ya Kondomu yahimizwa

Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu yeye anasema kuwa ni muhimu kwa Watanzania kudumisha utamaduni wa kutumia Kondomu pindi wanaposhiriki ngono ili kujikinga na maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI na kuepuka kupoteza nguvu kazi ya Taifa kutokana na UKIMWI.

Babu litoa wito huo Mei 10, mkoani Kilimanjaro alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara ya Mkoa huo wakati akitambulisha Kampeini ya Kili Challenge kwa mwaka 2023 yenye lengo la kuchangia jitihada za mwitikio wa UKIMWI nchini.

Anasema maambukizi ya VVU na UKIMWI bado ni tatizo nchini ambapo tawimu zinaonesha uwepo wa ongezeko la Maambukizi mapya ya VVU hususan kwenye makundi maalum pamoja na kundi la vijana.

“Jamii inajisahau sana na kufanya mchezo kwa madai ya kwamba ni ajali kazini, kuna kudai kuwa UKIMWI umeisha, hili jambo sio zuri kwani tunakuwa tunajitakia wenyewe, ni vizuri wote tukafahamu na kujua kuwa UKIMWI bado upo kwa mujibu wa takwimu alizotoa Mkurugenzi wa TACAIDS na niwajibu wa kila mmoja kujikinga,” anasema Babu.

SOMA PIA:

Amesema kwa hali halisi maambukizi ya VVU bado yapo nchini na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wanaendelea kupanga na kutekeleza afua mbalimbali za kitabibu na zisizoza kitabibu kwenye mwitikio wa UKIMWI, ambapo kumekuwa na mafanikio makubwa ya kupungua kwa ushamiri wa VVU nchini.

“Pamoja na mafanikio haya yaliyowezeshwa na wadau kutoka nchi mbalimbali na taasisi za kimataifa, kwa sasa ufadhili kutoka nje umepungua, hivyo kama nchi hatuna budi kubuni mikakati ya kutafuta raslimali za ndani kwa ajili ya mwitikio wa VVU na UKIMWI ili kupunguza au kuondoa utegemezi wa vyanzo vya nje na kuwa na vyanzo vyetu vya ndani,” anasema Babu.

Naye Makamu wa Rais wa Anglo Gold Ashanti, Simon Shayo anahimiza wafanyabiashara nchini kuunganisha nguvu ya pamoja katika kuhakikisha kuwa janga hilo linabakii kuwa historia ifikapo 2030 kama yalivyo malengo ya kidunia.

“Kwa ujumla bado kuna makundi mengi ambayo yapo hatarini na yanahitaji kufikiwa na afua mbalimbali za UKIMWI, na kwa bahati mbaya makundi hayo ni yale ambayo ndio nguvu kazi ya Taifa, miongoni mwa hayo ni makundi ya vijana, wachimbaji wadogo, wavuvi na madereva wa masafa marefu.

“Hivyo wafanyabishara na wengine katika nyanja mbalimbali ni muhimu kupaza sauti kwa pamoja katika kuhakikisha kwamba tunaongeza raslimali fedha ili kupambana na VVU,” anasema Shayo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img