15.8 C
New York

Dk. Tulia awataka watanzania kuulinda Muungano kwa wivu

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dk. Tulia Ackson, amesema ni wajibu wa kila mtanzania kuhakikisha anailinda kwa wivu wote tunu ya Muungano iliyoanzishwa na waasisi wa taifa hilo.

Dk. Tulia ameyasema hayo leo Aprili 25, 2025 wakati akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Pwani  katika  mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Kibaha ikiwa ni sehemu ya shughuli za Maadhimisho ya Miaka 61 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanyika katika mkoa huo.

Amemshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan,  kwa namna ambavyo amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha anasimamia maendeleo katika nyanda zote za bara na visiwani.

“Tanzania haiwezi kuwepo bila Muungano, Muungano huu umejengwa katika misingi imara umedumu na utaendelea kudumu. Kila mmoja wetu anapaswa kutafakari matendo na maneno yake yawe chachu ya kudumisha Muungano wetu, niwahakikishie kwamba Bunge litaendelea kuwa daraja katika pande zote mbili ili kuhakikisha Muungano unazidi kuwa madhubuti, unadumu na kuwa imara zaidi,” amesisitiza Dk. Tulia.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img