22.9 C
New York

Hapi: Matumizi ya mirungi yanaharibu Taifa

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

KATIBU Mkuu wa Umoja wa Wazazi Tanzania Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ally Salum Hapi (MNEC) amekemea vikali matumizi ya dawa za kulevya aina ya mirungi na bangi kwa vijana kote nchini huku akiagiza hatua stahiki kuchukuliwa ili kudhibiti hali hiyo ambayo inaangamiza nguvu kazi ya taifa na kurudisha nyuma maendeleo ya familia na Taifa kwa ujumla

Hapi amesema hayo Mei 8, 2024 akiwa katika kijiji cha Mnenia katika Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Dodoma, amesema matumizi ya mirungi katika eneo hilo na maeneo yote nchini hayakubaliki na yanapaswa kupingwa kwa nguvu zote ili kuwa na vijana wanaweza kuzalisha na kusimamia familia zao tofauti na ilivyo kwa baadhi vijana walioingia katika wimbi la uraibu wa madawa ya kulevya.

“Tunataka kuijenga nchi, tunataka kuijenga kondoa lakini hatuwezi kuijenga kondoa kwa kuwa na vijana tegemezi walioharibu maisha yao kwa kuingia na kujihusisha na vitendo viovu vya uvutaji wa mirungi, alisema mirungi inaharibu kabisa akili inaharibu familia ndoa nyingi zinaharibika kwa sababu vijana hawawezi kutekeleza majukumu yao ya kusimamia na kuendeleza familia tunapaswa kuikemea kwa nguvu zetu zote ili vijana wetu wajikite katika kufanya shughuli za maendeleo,” amesema Hapi.

Kuhusu suala la elimu Hapi amewataka wazazi kuwekeza kwa kusomesha watoto wao kwani ndiyo msingi wa maendeleo jamii na taifa

“Niwasihi sana ndugu zangu wekezeni kwa watoto hakikisheni watoto wanasoma anapata elimu ili tupate akina Hapi wengine,akina Dkt Ashatu Kijaji na wengine kwa ajili ya maendeleo ya Kondoa na Taifa letu lakini tukiacha watoto waendelee kuvuta madawa ya kulevya tutaendelea kuwa watumwa na watu tusio na tija hilo ni muhimu kulizingatia kwa kila mmoja wetu,” amesema Hapi.

Hoja hiyo ya mirungi imeungwa mkono na Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Dk. Ashatu Kijaji ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara pamoja na mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Dodoma, Samwel John Malecela ambao kwa pamoja wameungana kukemea vitendo hivyo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img