1.6 C
New York

Mwandishi Gazetini ang’ara tuzo za Merck Foundation

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Mwandishi wa Habari, Tulinagwe Malopa, anayefanyakazi na Tovuti ya GAZETINI (www.gazetini.co.tz) jijini Dar es Salaam inayomilikiwa na Gazetini Communications ameng’ara katika Tuzo za Merck More than A Mother (Diates and Hypertension) Media Recognation Award 2023 zinazotolewa na Wakfu wa Merck Foundation-Ujerumani.

Katika Tuzo hizo zilizotangazwa na Mkurugenzi Mkuu wa Seneta, Dk. Rasha Kelej, Aprili 19, mwaka huu, Tulinagwe ameibuka mshindi wa tatu kwa upande wa vyombo vya habari vya mtandaoni(Online Category) Afrika Mashariki.

Akizungumza na GAZETINI baada ya kutangazwa kushika nafasi hiyo, Tulinagwe amesema tuzo hiyo imempa chachu ya kuendelea kufanya kazi nzuri zinazogusa maisha ya watu.

“Nimeibuka mshindi wa tatu kwa upande wa waandishi wa habari wa Afrika Mashariki katika kipengele cha vyombo vya habari vya mtandaoni (Online category). Hii ni tuzo ya kutambua mchango wangu katika kuimarisha afya hususan mapambano dhidi ya ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu kwa mwaka 2023.

“Hivyo, kupata tuzo hii kwangu imenipa chachu ya kuendelea kupambana zaidi kwa kufanya kazi zinazogusa maisha ya watu na jamii kwa ujuma,” amesema Tulinagwe.

Tulinagwe ameitaja habari iliyompa ushindi huo kuwa ilihusu namna ya kuzuia kisukari na shinikizo la damu na hatua za kugundua mapema magonjwa hayo ya kiafya.

Akizungumza wakati wa kutangaza washindi hao, Dk. Rasha amesema vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kusaidia jamii zao kupunguza na kuondoa unyanyapaa kwa watu waliokosa watoto na ukeketeji.

“Tunahimiza wanahabari kuendelea kuelimisha jamii kuhusu magonjwa haya ili watu wawe na mtindo bora wa maisha kwa kuepuka magonjwa haya,” amesema Dk. Rasha.

Tuzo hizo zimetolewa kwa waandishi wa habari katika nchi mbalimbali duniani ambao walikuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu ya afya pamoja na uzazi.

Washindi wengine walikuwa ni Lucy John Bosco (Mwananchi Online), mshindi wa pili, Dorcas Wangir, (Citizen TV) – Kenya na Veronica Romwald wa Blog ya Matukio na Maisha akiibuka pia mshindi wa tatu.

Washindi wa Tuzo hizo ambazo zilianza kutolewa tangu mwaka 2017, kila mmoja atajinyakulia zawadi fedha kunzia Dola 500 pamoja na Medali kutoka kwa Wakfu huo wa Merck Foundation.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img