2.9 C
New York

Baraza la Wafanyakazi TACAIDS lafanyika na kupata viongozi wapya

Published:

Na Nadhifa Omar, TACAIDS

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dk. Jerome Kamwela, ameongoza kikao cha Baraza la wafanyakazi la Tume hiyo, kilichofanyika Februari 17, 2024 jijini Dodoma, ambapo alichukua nafasi hiyo kuongoza uchaguzi wa upatikanaji wa Katibu na Katibu msaidizi.

Mmoja wa washindi wa wafanyakazi bora, Geofrey Mabu akikabidhiwa Cheti na fedha Taslim, anayempongeza ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Jerome Kamwela, aliyesimama katikati ni Mwakilishi wa TUGHE Taifa na mjumbe wa kamati ya utekelezaji TUGHE Taifa, Dk. Allan Masanja na Mwisho kabisa Naibu Katibu wa Baraza la wafanyakazi TACAIDS, Jacqline Lema.

Katika Uchaguzi huo majina pendekezwa yalikuwa ni mawili ambayo ni Jaqline Lema na Dk. Hassan Ishabairu, baada ya kura kupigwa, Dk. Hassani Ishabairu alishinda kuwa Katibu wa Baraza la wafanya kazi la Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania -TACAIDS.

Baadhi ya watumishi walioshiriki kwenye kikao cha Baraza la wafanyakazi la TACAIDS kilichofanyika Februari 16,2024 jijini Dodoma.

Baada ya uchaguzi huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Jerome Kamwela, aliwataka wajumbe wa baraza la wafanyakazi la TACAIDS kushiriki kikamilifu kwa kuchangia na kujadili hoja muhimu  zitakazopelekea uboreshaji na ufanisi wa majukumu ya Tume.

Amesisitiza kuwa kikao hiki ni muhimu kwa taasisi yetu hivyo kila mtumishi azungumze bila hofu kwa lengo la kuboresha utendaji kazi  katika maeneo yetu na kuleta umoja, mshikamano na upendo katika maeneo ya kazi.

Mkurugenzi wa fedha na Utawala, Yasin Abas akifafanua maswauala ya Kiutumishi baada ya kuwasilisha Bajeti ya Idara yake.

Kupitia kikao hicho wafanyakazi bora tisa wa TACAIDS wa mwaka 2023 wamepatiwa zawadi kwa mujibu wa taratibu za chama cha wafanyakazi.

Aidha, Mkurugenzi wa Idara ya Sera, Mipango na Utafiti, Godfrey Godwin aliwasilisha Mapitio ya utekelezaji wa Bajeti ya Tume ya mwaka 2022/23, Mapitio ya Utekelezaji wa Bajeti ya Tume ya mwaka 2023/24 kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia Julai hadi Desemba 2023 na Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Tume ya mwaka  wa Fedha 2024/25.

 Wakuu wa Idara na vitengo wamewasilisha mipango ya bajeti ya Idara zao ambayo wameipanga kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu ya Tume mwaka wa fedha 2024/25 ambapo wajumbe walipata nafasi ya kujadili na kupitisha mipango hiyo.

Mkurugenzi wa Idara ya Sera, Mipango na Utafiti, Godfrey Godwin aliwasilisha Mapitio ya utekelezaji wa Bajeti ya Tume ya mwaka 2022/23, Mapitio ya Utekelezaji wa Bajeti ya Tume ya mwaka 2023/24 kwa kipindi cha nusu mwaka kuanzia Julai hadi Disemba 2023 na Mapendekezo ya Mpango na Bajeti ya Tume ya mwaka wa Fedha 2024/25. Kwenye Baraza la Wafanyakazi la TACAIDS lililofanyika Februari 16, 2024 jijini Dodoma.

Baada ya Mawasilisho hayo Baraza la wafanyakazi limepitisha bajeti hiyo ya mwaka 2024/25 kwa hatua  nyingine zaidi, Mwakilishi wa TUGHE Taifa na mjumbe wa kamati ya utekelezaji TUGHE Taifa Dr. Allan Masanja amesema TACAIDS imefanya kazi nzuri kupitia taarifa zake ilizowasilisha na amewapongeza kwa ubunifu katika utekelezaji wa majukumu yake.

Amewataka kutekeleza bajeti kwa ufanisi ambayo wameiandaa kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwani pamoja na kazi kubwa ambayo inatekelezwa na Tume hiyo kwa ufanisi bado kuna kazi kubwa ya kufanya kwakuwa jamii kubwa bado inahitaji huduma kutoka TACAIDS.

“Tunawapongeza mnavyojitahidi kuhakikisha Taifa letu linapata elimu ya kujikinga na maambuzi ya VVU lakini bado kuna jamii kubwa ambayo bado inawahitaji kupata huduma yenu,hasa sehemu za vyuo na maeneo yenye uhatarishi wa kupata maambukizi ya vvu,” alisema Allan Masanja.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Jerome Kamwela akizungumza na wajumbe wa baraza la wafanyakazi lilofanyika Februari 16, 2024 jijini Dodoma.

Aidha, amewataka watendaji wa TACAIDS kudumisha upendo na nidhamu mahala pa kazi na kuchapa kazi ili malengo yaliyowekwa kufikia asilmia 100, ikiwa ni pamoja na  kutoruhusu vishawishi vya rushwa kwani ni adui wa haki .

Katibu wa chama cha wafanyakazi Mkoa wa Dodoma (TUGHE), Samweli Nyungwa amewapongeza wafanyakazi wote waliopatiwa vyeti na zawadi za wafanyakazi bora na kuwataka wahakikishe zawadi hizo wanaendelea kuzitendea haki kwa kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img