7.1 C
New York

Rostam kuanza kuzalisha umeme Zambia

Published:

*Kuanza kwa kuwekeza Bilioni 250

Na Mwandishi Wetu, Lusaka

Mfanyabishara wa Kimataifa, Rostam Aziz, kupitia kampuni yake ya Taifa Group, ameingia nchini Zambia ambako ameanza kuwekeza kwenye sekta ya uzalishaji umeme kwa kutumia gesi.

Chini ya kampuni yake tanzu ya Taifa Gas, Rostam Aziz amewekeza kiasi cha awali cha dola milioni 100 katika uwekezaji huo kwa kushirikiana na kampuni ya Zambia iitwayo Delta Marimba.

Kampuni hizo mbili zimeunda kampuni ya ubia ya Taifa Marimba ambayo ndiyo inafanya uwekezaji huo huku mtambo wa kwanza wa kuzalisha umeme kwa kutumia gesi ukijengwa katika eneo la Kasama nchini Zambia.

Uwekezaji huo umemfurahisha Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, ambaye alimhakikishia Rostam na timu yake ushirikiano kutoka katika serikali yake.

Rostam ametoa kauli hiyo Ijumaa Oktoba 20, 2023 wakati yeye na timu yake walipomtembelea Ikulu jijini Lusaka, Zambia ili kumweleza kuhusiana na ubia na uwekezaji huo.

Rais Hichelema na Rostam Aziz walisistiza katika kikao hicho kuwa ubia wa aina hiyo ni moja yan jia nzuri za kuhakikisha Afrika inaondokana na utegemezi kutoka nchi.

Aidha, wawili hao walibainisha kuwa ubia awa aina hiyo utaipatia Afrika nguvu ya kutumia rasimali zake kwa ajili ya uzalishaji badala ya rasim, imali hizo kuzinufaisha nchi nyingine.

Rais Hichelema alisema hivi sasa nchi yake inaangalia namna ya kuongeza uzalishaji umeme kwa kutumia njia mbadala wa maji kutokana na athari za mabadiliko ya taifa nchi.

“Kwa hiyo kuja kwa Taifa Marimba na kuwekeza katika uzalishaji umeme kwa kutumia gesi kunaendana na mtazamo wetu, Tunaziunga mkono juhudi hizi na ningewahimiza mfanye haraka kukamilisha uwekezaji huu,” alisema.

Kwa mujibu wa Aziz, uwekezaji wa awali unalenga katika kubadiliahs mitambo inayotumia dizeli ili iweze kuzalisha umeme kwa kutumia gesi lakini hapo baadaye uwekezaji utaelekezwa pia kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu za upepo na jua.

“Pia tutawekeza katika maeneo mengi nje ya uzalishaji umeme kwani tumeona Zambia kuna fursa nyingi za uwekezaji,” alisema.

Alisema Taifa Marimba imeamua kufanya uwekezaji huo kwa dhamira ya kutaka kudumisha uhusiano wa kidugu na wa muda mrefu baina ya nchi hizo mbili.

“Pia tunafanya hivi tukiamini kuwa ubia baina ya kampuni za Afrika utatupatia nguvu ya kuweza kufanya mambo mengi makubwa sisi wenyewe bila kumuangalia mtu mwingine kutoka nje ya Bara letu. Tunaamini kuwa kwa kuunganisha nguvu tunaweza kutatua matatizo yetu mengi huku tukihakikisha rasilimali zetu zinatumika kama malighafi hapa hapa nchini badala ya kuwanufaisha watu wengine wa nje,” alisisitiza Aziz.

Rais Hichelema aliunga mkono hilo akibainisha kuwa iwapo kampuni za Afrika zitafanya kazi pamoja zinaweza kulifanya bara la Afrika kuachana na kuzalisha malighafi kwa ajili yan chi nyingine nje ya bara hilo.

“Mathalani, uwekezaji huu unaofanyika hapa utaongeza ukuaji wa uchumi lakini pia kuna ajira zitatengenezwa katika mnyororo huu wa thamani,” alisema.

Zambia inakuwa nchi ya pili kwa Rostan na kampuni yake ya Taifa Gas kuwekeza katika ukanda wa SADC kwani mapema mwaka huu kampuni hiyo iliingia nchini kenya ambako inajenga kiwanda cha kuchakata gesi ya kupikia jijini Mombasa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img