22.9 C
New York

Zaidi ya Milioni 200 kudhibiti wanyama wakali Serengeti

Published:

Na Malima Lubasha, Gazetini

SHIRIKA la Frankfurt Zoological Society(FZS) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara,wamezindua Mradi wa kudhibiti  wanyama wakali na waharibifu katika vijiji 15 vinavyopa kana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Meneja wa Operesheni kutoka FZS, Edmund Tobico, akizungumzia mradi huo Juni 6, 2023 wilayani Serengeti amesema utatekelezwa kwa muda wa miezi 16 chini ya ufadhili wa  Elphant Criss Fund (ECF) katika vijiji hivyo kwa thamani ya dola 95,000 sawa na Sh 225,532,565.

Amesema mradi huo utapunguza changamoto hizo na tayari limenunuliwa gari ambalo halitakiwi kufanya kazi nyingine zaidi ya hiyo pia vitanunuliwa vifaa kwa ajili ya vikosi kazi vya kuzuia wanyama waharibifu kutoka maeneo husika.

“Vile vile tutakarabati ofisi, kutoa ajira ambapo kabla ya mradi huu kulikuwa na mradi mwingine ambao ulisaidia kuimarisha mazizi na vihenge maana tembo walikuwa wakikosa mazao shambani wanayafata nyumbani,” amesema Tobico.

Aidha,Tobico ameongeza kuwa watajenga shamba darasa la kilimo cha pilipili kama njia ya kudhibiti wanyama kama tembo na kuwasaidia wananchi kuongeza kipato na kupata kutoa mafunzo kwa ajili ya vikosi kazi kufanya vizuri kazi zao katika vijiji hivyo na vile 7 vya Ikona WMA.

Mradi huo umepewa gari kwa ajili ya kufanya dolia katika vijiji 22 vya kando kando ya hifadhi ya Serengeti kwa kuwa na vikosi kazi vya udhibiti.

Afisa Wanyamapori Halmashauriya Wilaya ya Serengeti, John Lendoyan amesema kuanzishwa kwa mradi huo ni kutanua wigo wa ulinzi kwani awali nguvu kubwa ilikuwa katika vijiji 7 vya Ikona WMA kwa sasa vikundi 51 vya Elephant Control Group vimeundwa katika vijiji 36 ambapo aliomba wadau mbalimbali wajitokeze kuisaidia Serengeti Problem Animal Control Unit (SEPACU) ili waweze kufika maeneo mengi zaidi.

Amesema kuwa sababu kubwa ya migogoro ni baada ya kuimarika kwa uhifadhi, kuongezeka kwa idadi ya watu na wanyama, msukumo wa kiikolojia na kibailojia, mabadiliko tabia nchi, kutozingatia matumizi bora ya ardhi,ongezeko la kambi za kitalii, kuvamiwa kwa shoroba hivyo kuna haja ya kuanzishwa kwa WMA nyingine kuongeza fursa zaidi.

Afisa Utalii Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Upendo Massawe ameshauri maeneo ya pembezoni wananchi walime mazao ambayo hayapendwi na wanyama waharibifu na kuomba kuanzishwa kwa WMA nyingi ne utasaidia fursa za kiuchumi kwani kambi nyingine zitakuwa nje badala kujazana  ndani.

Akizindua mradi na kukabidhi gari na vifaa kwa ajili kikozi kazi, Profesa Mshirikikuka, Chuo Kikuu cha WASEDA Japani, Iwai Yukino amewataka watumishi waliopewa dhamana kutumia vizuri mali hiyo ya umma na kwamba mradi huo uwe jibu la baadhi ya changamoto zilizopo kati ya wanyama na binadamu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img