Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Mshauri wa Rais Samia Suluhu Hassan katika masuala ya afya, Profesa Mohammed Janabi, ameshinda nafasi ya Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika katika uchaguzi uliofanyika leo Mei 18, 2025, Geneva, Uswizi.
Prof. Janabi ametetea nafasi hiyo iliyokuwa inashikiliwa na Mtanzania marehemu Dk. Faustine Ndegulile.


Prof.Janabi amewashinda wagombea wengine wanne ambao ni N’da Konan Michel ( Ivory Coast), Mohammed Lamine (Guinea)Dk Boureima Hama Sambo (Niger) na Professa Moustafa Mijiyawa wa Togo.