25.1 C
New York

Serikali ya Marekani kutoa Dola milioni moja mapambano dhidi Mpox

Published:

Na Mwandishi Wetu

Serikali ya Marekani kupitia Kituo cha Kudhibiti Maradhi (CDC), imetangaza kutoa msaada wa karibu dola milioni moja kwa ajili ya kuimarisha ufuatiliaji na udhibiti wa kuenea kwa ugonjwa wa mpox nchini.

Fedha hizo zitasaidia Wizara za Afya za Tanzania Bara na Zanzibar katika jitihada zao za kufuatilia, kugundua na kudhibiti maambukizi.

Ufadhili huo, uliotolewa na Kituo cha Kudhibiti Maradhi cha Marekani (CDC)utalenga katika maeneo muhimu kama vile kuimarisha ufuatiliaji wa kubaini makundi mapya ya maambukizi.

Pia kupanua hatua za kuzuia na kudhibiti maambukizi katika vituo vya kutolea huduma za afyaKuongeza uwezo katika vituo vya kuingilia wageni ili kuzuia kuenea kwa mpox, kutoa vifaa muhimu vya maabara,kusaidia Vituo vya Matibabu ya Dharura (EOCs) ili kuboresha uchambuzi wa data na mawasiliano, ikiwemo kuandaa taarifa kuhusu hali halisi ilivyo zinazoonesha takwimu za kidemografia na data za matukio yaliyoripotiwa katika mikoa mbalimbali, kuimarisha juhudi za mawasiliano ya umma na uelimishaji.

Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Andrew Lentz amesema kupitia uwekezaji huo Serikali ya Marekani inathibitisha tena dhamira yake ya dhati ya kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuimarisha uwezo wa Tanzania kukabiliana na milipuko ya maradhi.

“Serikali ya Marekani inajivunia kuchangia utaalamu wa kiufundi, uwekezaji, na msaada wa moja kwa moja kwa ajili ya kulinda afya na usalama wa wananchi wa Marekani na Tanzania.

“Mpox husababisha dalili kama vile upele unaouma, uvimbe wa mitoki, homa, maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli, na uchovu. Ingawa watu wengi hupona bila matatizo makubwa, baadhi yao huweza kupata maradhi makali.

“Marekani inajivunia kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuimarisha jitihada za kupambana na mpox na kulinda afya na ustawi wa Watanzania na Wamarekani katika vita ya kimataifa dhidi ya mpox.

“Kwa kuunga mkono jitihada za afya za kimataifa, tunaifanya Marekani kuwa salama na imara zaidi dhidi ya tishio la magonjwa yanayoibuka,” ameeleza.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img