7.9 C
New York

Miradi ya TUI Care Foundation kuboresha misitu kwa utalii endelevu

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Misitu ina mchango mkubwa katika sekta ya utalii, ikivutia mamilioni ya wageni kila mwaka na kuchangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa jamii za wenyeji. Ikiwa inashughulikia zaidi ya 30% ya ardhi ya dunia, misitu hutoa fursa nyingi za burudani. Kutambua thamani yake katika maendeleo ya utalii endelevu.

TUI Care Foundation inapanua miradi yake ya uhifadhi wa misitu katika Gran Canaria, Zanzibar, na Kenya. Miradi hii inalenga kukuza suluhisho endelevu za utalii zinazowanufaisha watu wa maeneo husika pamoja na mazingira.

Katika Zanzibar, Hifadhi ya Taifa ya Msitu wa Masingini, karibu na eneo la Urithi wa Dunia la Stone Town, inakabiliwa na hatari ya ukame wa mijini na ukataji miti. Mradi wa TUI Forest Zanzibarunalenga kuunda eneo la kinga kati ya mji na msitu kwa kupanda zaidi ya 63,000 ya miti ya asili.

Pia, mradi huu unatoa elimu ya mazingira kwa vijana na jamii ili kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa misitu. Kwa kushirikiana na Kawa Foundation, mradi huu unakuza utalii wa mazingira kama vile matembezi na safari za baiskeli ili kuwavutia watalii na kuongeza kipato kwa jamii za wenyeji.

Nchini Kenya, Taita Hills Wildlife Sanctuary, eneo muhimu kwa ekolojia na utalii, limeathiriwa na ukame wa muda mrefu, hali inayosababisha mmomonyoko wa udongo na kupotea kwa mimea. TUI Forest Kenya, kwa kushirikiana na Taita Taveta Wildlife Conservancies Association, inatekeleza mradi wa kupanda miti 40,000 na kurejesha zaidi ya hekta 24 za misitu katika eneo muhimu la ukanda wa mto. Mradi huu pia una kitalu cha miti kinachoendeshwa na jamii na kampeni ya “Acha Alama ya Kijani”, inayohamasisha watalii kushiriki katika upandaji miti na kusaidia jitihada za uhifadhi wa mazingira.

Katika Gran Canaria, moto mkubwa wa msituni wa mwaka 2019 na ukataji miti wa kihistoria vimeathiri kwa kiasi kikubwa bayoanuwai na ubora wa udongo. TUI Forest Gran Canaria, kwa kushirikiana na Fundación Canaria para la Reforestación (FORESTA), inalenga kurejesha msitu kwa kupanda miti 3,000 ya asili, kutoa ajira, na kuwashirikisha zaidi ya 700 ya wahusika wa kujitolea katika shughuli za upandaji miti. Wageni wa visiwa hivyo wamepata fursa ya kupanda miti kama sehemu ya jitihada za kupambana na mmomonyoko wa udongo na ukame.

TUI Care Foundation pia imezindua Forest February’, mwezi maalum wa shughuli za urejeshaji wa misitu, ikihimiza usimamizi wa misitu unaoongozwa na jamii, pamoja na utalii wa kilimo endelevu, ili kulinda mifumo ya ikolojia kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img