23.8 C
New York

Serikali yasamehe wadaiwa faini za maji, yataka wananchi warejeshewe huduma

Published:

Na Mwandishi Wetu

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso ametangaza msamaha wa faini zote kwa wananchi waliokuwa wakidaiwa na Mamlaka za Maji nchini, hatua inayolenga kuwapunguzia mzigo wa gharama na kuwawezesha kurejeshewa huduma za maji.

Aweso ametangaza msamaha huo leo Mei 8, 2025, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa fedha 2025/2026, bungeni jijini Dodoma.

“Ninapenda kutoa salamu za wizara kwa wananchi wote wenye faini kuwa Mama Samia Suluhu Hassan amesamehe faini hizo. Wafike katika Mamlaka za maji kuanzia sasa hadi Mei 31, 2025, ili kupewa utaratibu wa kurejeshewa huduma ya maji,” amesema.

Pia amesisitiza kuwa wateja wote waliokatiwa maji kutokana na madeni, wanatakiwa kufika katika ofisi za mamlaka husika ili kupewa utaratibu wa ulipaji wa madeni yao na kurejeshewa huduma.

Aidha ameeleza kuwa huduma ya maji vijijini sasa inawafikia asilimia 83 ya wananchi, ikilinganishwa na asilimia 79.6 mwezi Desemba, 2023, wakati mijini huduma imeongezeka  na kufikia asilimia 91 kutokana na kukamilika kwa miradi 68 ya maji, ambayo imewanufaisha zaidi ya wananchi milioni tatu.

Ameliomba Bunge kuidhinisha  zaidi ya Shilingi Sh 1.01 trilioni kwa mwaka wa fedha 2025/2026 

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img