Na Ramadhan Hassan,Dodoma
Serikali imepanga kufunga mfumo wa kielektroniki ambao unawezesha magari kupimwa kwenye mizani bila usaidizi wa mtu (operator)
Hayo yameelezwa leo bungeni Machi 5,2025 jijini hapa na Waziri wa Ujenzi,Abdallah Ulega wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2025-2026.
Waziri Ulega amesema Serikali kupitia TANROADS imeendelea kutekeleza ilani ya CCM kwa kujenga na kuboresha mizani ya kupima magari ili kulinda barabara zisiharibike mapema na kuimarisha udhibiti wa uzito wa magari na kupunguza muda wa upimaji.

Amesema Wizara inajenga mizani ya kisasa ambayo hutoa taarifa ya mwenendo mzima wa hali ya mizani wakati gari linapimwa ili kupata vipimo sahihi katika mizani.
Ulega amesema hadi sasa, ‘Load Cell’ za kidigitali zimefungwa katika mizani 10 ambayo ni Mpemba, Njuki, Mikese North, Mikese South, Mikumi North, Nala, Makuyuni, Mutukula, Mingoyo na Himo.
“Hadi sasa, mizani 20 ya kupima magari yakiwa kwenye mwendo (Weigh-in-Motion) imefungwa katika vituo vya mizani vya Vigwaza, Mikese, Mikumi, Wenda, Mpemba, Nala, Njuki, Kimokouwa, Dakawa na Rubana,”amesema Ulega.