22.7 C
New York

Balile awashauri waandishi wa habari wanaoripoti kesi ya Lissu

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile, ameshauri waandishi wa habari kuwa na alama za utambuzi wakati wa kuripoti kesi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo  Mei 2, 2025, katika ofisi ya taasisi hiyo jijini Dar es Salaam,  amesena miongoni mwa alama hizo ni kuvaa jaketi la uandishi wa habari na kitambulisho cha kazi.

“Baada ya zile purukushani pale mahakamani, nikasema haiwezekani mwandishi akazuiwa kufanya kazi yake.

“Nilikutana na Afande Jumanne Muliro ( Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam) na tukakubalia kuzuia waandishi Kisutu sio jambo jema. Tukakubaliana siku ya kesi ya Lissu tarehe 6 Mei waingie wote lakini kuwe na utambuzi,” amesema,” Balile.

Ameeleza kuwa mwandishi hapaswi kuzuiwa kufanya kazi yake ya kukusanya, kuchakata na kuhabarisha umma, hata amesema wanahabari wanapaswa kufika mahakamani mapema kwa kuwa, chumba kikijaa hawatopata nafasi.

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Dar es Salaam, Bakari Kimwanga amesema, wanahabari wanapaswa kuhakikisha wanakuwa salama wakati wa kazi.

“Jambo la usalama ni la kwanza kisha kazi (habari), jukumu la usalama ni lako mwanahabari,” amesema.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img