2.6 C
New York

REA kusambaza mitungi 22, 000 ya gesi Tabora kwa Sh milioni 455

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetenga kiasi cha shilingi milioni 455.7 kwa ajili ya kusambaza mitungi ya gesi 22,785 mkoani Tabora, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini.

Hayo yameelezwa leo, Novemba 22, 2024, na Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala wa REA, Advera Mwijaje, wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya REA mkoani humo.

Mwijaje alitaja wilaya zitakazonufaika na mradi huo kuwa ni Uyui, Urambo, Nzega, Sikonge, Kaliua, Igunga, na Tabora Mjini. Alisema mpango huo unalenga kuchochea matumizi ya nishati safi na kupunguza utegemezi wa kuni na mkaa, ambavyo vinaathiri mazingira.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Tabora, Dk. John Mboya, ameipongeza REA kwa jitihada hizo, akisema nishati safi ya kupikia ni ajenda ya kimataifa na ni muhimu kuelimisha jamii kuhusu matumizi salama na endelevu ya nishati hiyo.

“Natoa shukrani kwa REA kwa hatua hii muhimu ya kusambaza mitungi ya gesi na pia kufikisha umeme vijijini. Ni muhimu kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali, yakiwemo makampuni makubwa, ili miradi hii iwe na manufaa kwa wananchi wengi zaidi,” alisema Dk. Mboya.

REA pia inaendelea kutekeleza miradi mingine mkoani Tabora, ikiwa ni pamoja na kusambaza umeme katika vijiji na vitongoji, jambo linaloimarisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img