8.3 C
New York

Mwenge wa Uhuru kukagua miradi yenye thamani ya Sh Trilioni 8.5 Pwani

Published:

Na Grace Mwakalinga, Gazetini-BAGAMOYO

ZAIDI ya miradi 120 yenye thamani ya sh. Trilioni 8.5  kati yake, miradi 18 itawekwa jiwe la msingi, 22 itazinduliwa na 86 itakaguliwa na mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo tayari imeanza kukimbizwa mkoani Pwani.

Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amepokea mwenge huo  wa Uhuru kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Morogoro, Adam Malima ambapo makabidhiano yalifanyika  eneo la Bwawani mkoani Pwani.

Kunenge amesema mwenge huo wa Uhuru utatembelea, kuweka jiwe la msingi na kuzindua miradi 126 ya maendeleo katika wilaya saba na halmashauri tisa za mkoa wa Pwani.

Amesema kati  fedha hizo Sh trilioni 8.5 zilizotumika kukamilisha miradi mbalimbali, bilioni 13.6 zilitoka serikali kuu, Halmashauri za wilaya bilioni 2.3, nguvu za wananchi na wawekezaji trilioni 8.5 na wadau wa maendeleo bilioni 14.6.

“Kwa kuzingatia ujumbe  wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024, unaosema Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu, kwa kipindi cha 2023/2024 mkoa umeweka lengo ya kupanda miti milioni 13.5.hadi kufikia mwezi Juni 2024 na hadi sasa jumla ya miti milioni 8.8 imepandwa kwenye maeneo mbalimbali ya mkoa huu,” amesema Kunenge.

Ukiwa wilayani Bagamoyo, Halmashauri ya Chalinze Mwenge wa Uhuru, umezindua barabara na ujenzi wa daraja  Kwamela -Lukwambe uliogharimu milioni 365.9 daraja   lililojengwa kwa Sh milioni 190.

Miradi mingine ujenzi wa shule ya awali na msingi ya Ridhiwani Kikwete, mradi uliotekelezwa kwa kutumia force account, ujenzi ambao ulitokana na shule ya awali na msingi Bwilingu A kuwa na msongamano wa wanafunzi 1984.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img