1.4 C
New York

TACAIDS yawataka wadau kushiriki upatikanaji fedha za Mwitikio wa UKIMWI

Published:

Na Nadhifa Omary, Gazetini-Dodoma

Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), imehimiza wadau kutoa ushirikiano kwa maoni na mawazo yao chanya ambayo yataboresho mkakati wa ukusanyaji fedha kwa ajili ya mwitikio wa UKIMWI nchini (HIV Sustainable Financing Framework) unaondaliwa na TACAIDS.

Mkakati huo unaandaliwa kwa ajili ya kuboresha njia za kukusanya rasilimali fedha zitakazosaidia utekelezaji wa shughuli za VVU na UKIMWI pamoja na utoaji wa huduma za UKIMWI kuwa endelevu hapa nchini, kwa kushirikisha wadau wa ndani ya nchini wakiwemo wadau kutoka kwenye sekta binafsi.

Akizungumza na washiriki katika kikao cha wadau cha kupitia rasimu ya mkakati huo kilichofanyika kuanzia Aprili 17 hadi 18, 202 jijini Dodoma leo Aprili 18,2024, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Jerome Kamwela, amesema kuwa kuekelea 2030 ambapo Dunia inatarajia kumaliza UKIMWI suala la upatikanaji wa raslimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za UKIMWI pamoja na utoaji wa huduma za UKIMWI kutoka katika vyanzo vya ndani ya nchi ni la kupewa kipaumbele kikubwa.

“Hivi sasa suala la UKIMWI ni la kila mmoja wetu hapa nchini, hivyo ni muhimu kwa pamoja tukaangalia ni kwa namna gani tutashirikiana ili kupata raslimali fedha kwa ajili ya Mwitikio wa UKIMWI kutoka katika vyanzo vya ndani,” alisema Dk. Kamwela.

Mkuu wa Kitengo cha Sheria cha TACAIDS, Devis Misingo akichangia mada kwenye kikao cha kupitia rasimu ya mkakati wa kukusanya fedha za Mwitikio wa UKIMWI nchini ‘HIV financing framework’. Kuhusu sheria inayomlinda mchangiaji raslimali fedha kwenye Mwitikio wa UKIMWI wakati wa kikao kilichofanyika jijini Dodoma.

Kuhusu hali ya UKIMWI nchini, Dk. Kamwela alifafanua kuwa utafiti uliozinduliwa Desemba mosi, 2023 ulionesha kwamba, watu elfu 60 wanapata maambukizi mapya kwa mwaka hapa nchini.

Wakati matarajio ilikuwa ifikapo mwaka 2020 maambukizi mapya yawe chini ya watu elfu 20 kwa mwaka hapa nchini, hivyo bado kuna kazi kubwa ya kufanya kuhakikisha rasilimali fedha zinapatikana ili kupambana na UKIMWI hapa nchini. Aliongeza kuwa, mkakati huo utasaidia pia kuonesha maeneo ya kipaumbele yatakayoleta matokeo ya haraka.

Dk. Kamwela ameongeza kuwa ili kufikia lengo la kumaliza UKIMWI ifikapo 2030 jitihada za mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI ikiwa ni pamoja na kubuni mbinu bora za utekelezaji wa afua za UKIMWI zinahitajika katika kuzuia maambukizi mapya na kumaliza vifo vitokanavyo na UKIMWI.

Amesema fedha nyingi bado zinahitajika katika utekelezaji wa shughuli za UKIMWI nchini ambapo kwa mwaka tunahitaji dola milioni 500 hadi 600.

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa TACAIDS, Godfrey Godwin akielezea namna Tume inavyoshirikiana na  wadau pamoja na Sekta binafsi katika kuhamasisha upatikanaji wa vyanzo vya raslimali  za Mwitikio wa UKIMWI nchini, alikuwa akichangia kwenye kikao cha siku mbili cha kupitia rasimu ya mkakati wa kukusanya raslimali za mwitikio wa ukimwi nchini.

Amefafanua zaidi kuwa hadi sasa asilimia 90 ya fedha kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za UKIMWI nchini zinategemewa kutoka kwa wafadhili wa nje ya nchi wakati tatizo la UKIMWI niletu.

Mwakilishi kutoka Mpango wa Taifa wa kudhibiti UKIMWI, Kifua kikuu na Magonjwa ya ngono – NASHCOP, Dk. Boniface Mlay ameshukuru jitihada zinazofanywa na TACAIDS ambaye ndiye mratibu wa shughuli za UKIMWI nchini na mwenye jukumu la kutafuta rasilimali kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za UKIMWI pamoja na utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI hapa nchini.

Dk. Boniface aliendelea kusema kwamba, fedha zinahitajika na asilimia 80 ya dawa na vifaa tiba vinaletwa na wafadhili, lakini uhitaji wa fedha bado ni mkubwa, na hivyo maoni ya kila mmoja hapa ni muhimu,  ili kuhakikisha tunapata huu Mkakati na kuona ni namna gani tunapata vyanzo vya kudumu vya fedha za Mwitikio wa UKIMWI.

Mtalaam wa UKIMWI kutoka UNICEF, John George akichangia umuhimu wa nchi kuwa na vyanzo vya ndani vya upatikanaji wa fedha za Mwitikio wa UKIMWI wakati wa kikao cha kupitia rasimu ya mkakati wa kukusanya fedha za mwitikio wa UKIMWI nchini.

Akizungumza kwa niaba ya wadau wa maendeleo, Dk. Mariam Ngaeje mtaalam wa haki ya afya ya uzazi na UKIMWI kutoka UNFPA amesema wadau wa maendeleo wanaendelea kuunga mkono na kutoa michango ya fedha na utaalam katika jitihada ambazo zinafanywa na serikali katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI  na kufika malengo yaliyowekwa ya kumaliza UKIMWI ifikapo 20230

Wote tunalenga katika kuhakikisha kwamba hatuna maambukizi mapya kama nchi na watu hawapati changamoto zinazoendana na upungufu wa kinga mwilini pamoja na vifo ifikapo 2030

Dk. Marim ameishukuru Serikali kwa jitihada zinazofanywa za kupata rasilimali fedha kutoka vyanzo vya ndani ili kufanikisha kila mtanzania anakuwa na afya njema na ustawi bora. ni kweli kuwa jitihada za serikali ni kwa ushirikiano na wadau wa maendeleo ikiwemo mashirika ya kimataifa. Tunajitahidi kuchangia kwenye kile ambacho serikali inakifanya kuhakikisha tunakuwa na fedha za ndani kwa ajili ya mwitikio wa UKIMWI.

Mkuu wa Ofisi za Kanda kutoka SIKIKA, Richard Msittu akichangia kichangia umuhimu wa kushirikisha sekta binafsi wakati wa kikao cha kupitia mkakati wa kukusanya fedha za mwitikio wa UKIMWI nchini.

“Tunategemea maarifa na uzoefu wenu vitatusaidia kuboresha mkakati huu na kupata vyanzo endelevu kwa ajili ya upatikanaji wa fedha za mwitikio wa UKIMWI, ikiwa ni pamoja na namna bora kushirikisha sekta binafsi katika kuchangia utekelezaji wa shughuli za UKIMWI nchini pamoja na utoaji huduma bora za VVU na UKIMWI nchini,”.

Mkuu wa kitengo cha Tiba na Matunzo kutoka NASHCop, Dk. Boniface Mlay akifafanua namna ambavyo upatikanaji wa fedha za ndani za Mwitikio wa UKIMWI zitakavyosaidia hasa katika ununuzi dawa na kupunguza utegemezi,wakati wa kikao cha rasmu ya mkakati wa kukusanya fedha za mwitikio wa UKIMWI nchini.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img