21 C
New York

Marufuku Pikipiki kubeba watoto walio chini ya miaka 9

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Kikosi cha Usalama Barabarani kimetangaza kuwa kuanzia wiki ijayo wakati shule zikifunguliwa, dereva wa Pikipiki maarufu kama bodaboda atakayebeba mtoto chini ya miaka tisa, atachukuliwa hatua za kisheria yeye na mzazi.

Sambamba na hilo, pia kimetangaza magari maalumu ya kubebea wanafunzi ambayo hayajafanyiwa ukaguzi hadi kufikia wiki ijayo wakati shule zinafunguliwa, yatafungiwa.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani chini, Ramadhan Ng’anzi ametoa maagizo hayo kuhusu usalama wa watoto barabarani leo Januari 5, 2024 wakati shule zikifunguliwa kuanza muhula wa kwanza wa masomo
2024.

“Wazazi wanaotumia bodaboda kuwapeleka na kuwarudisha shule watoto wao, wahakikishe watoto hao wana umri wa miaka tisa na kuendelea kama ana umri chini ya huo ampandishe bajaj,” – amesema Kamanda Ng’anzi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img