1.7 C
New York

Luhemeja awataka Madiwani kuwa Mabalozi wa Usalama na Afya

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Katibu Mkuu – Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhandisi, Cyprian Luhemeja amewataka madiwani wa Mkoa wa Dodoma kuwa mabalozi wa Usalama na Afya katika miradi yote wanayoisimamia na inayotekelezwa kwenye kata zao ili kulinda nguvu kazi dhidi ya magonjwa na ajali katika maeneo ya kazi.

Katibu Mkuu – Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhandisi, Cyprian Luhemeja akizungumza na Madiwani wa viti maalumu wa Mkoa wa Dodoma wakati akifunga mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi kwa madiwani hao yaliyoambatana na zoezi la upimaji wa magonjwa yatokanayo na kazi kwa madiwani hao. Kushoto kwake ni Mbunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Dodoma, Fatma Hassan Toufiq na kulia kwake ni Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda.

Luhemeja ametoa wito huo wakati akifunga mafunzo ya usalama na afya mahali pa kazi yaliyoandaliwa na OSHA  kwa madiwani wa viti maalumu, madiwani wanawake na wajasiriamali wanawake wa mkoa Dodoma yaliyoenda sambamba na zoezi la upimaji Afya wa magonjwa yatokanayo na kazi kwa madiwani  hao yaliyofanyika katika Ofisi za OSHA Dodoma.

“Mkoa wa Dodoma kwa sasa unamiradi mingi sana inayotekelezwa na serikali ikiwemo miradi ya ujenzi, maji, barabara, upanuaji wa mji n.k. na hii inaashiria kwamba kuna haja ya kuweka mifumo dhabiti ya kumlinda mfanyakazi dhidi ya vihatarishi vya vya magonjwa na ajali vinavyoweza kutokea wakati wa utekelezaji wa miradi hii ndio maana tumeamua kuendesha mafunzo haya ili yawasaidie katika kulinda usalama na afya za wafanyakazi katika miradi yote mnayoisimamia hivyo basi nawaagiza mkawe mabalozi wa OSHA katika maeneo yenu ya kazi,” alisema Luhemeja.

Katibu Mkuu huyo aliongeza na kuwataka OSHA kuendeleza program ya mafunzo haya kwa maeneo mengine ili kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa salama wakati wote wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Mbunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Dodoma, Fatma Hassan Toufiq akizungumza na madiwani wa viti maalumu wa Mkoa wa Dodoma wakati wa kufunga mafunzo yaliyoenda sambamba na zoezi la upimaji wa magonjwa yatokanayo na kazi kwa madiwani hao mkoani Dodoma.

Kwa upande wake Mbunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Fatma Hassan Toufiq amesema kuwa mafunzo haya kwa madiwani yamekuja muda muafaka kutokana na wingi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa huo.

“Nawapongeza sana waheshimiwa madiwani wote kwa mafunzo haya ambayo mmeyapata natarajia kuwa mtakapo rudi katika maeneo yenu ya kiutendaji ninyi ndio mtakuwa mabalozi wazuri wa kuitangaza OSHA kwamba kazi wanayoifanya ni kwaajili ya ustawi na maendeleo ya wafanyakazi wote katika maeneo ya kazi, Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe, Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassani imekuwa imetoa fedha nyingi za maendeleo katika mkoa wetu na kuna miradi mingi inatekelezwa ikiwemo Ujenzi wa Barabara,Ujenzi wa Reli SGR, na Bomba la Mafuta miradi hii inapita kwenye maeneo yetu hivyo sisi madiwani ni wajibu wetu kusimamia hilo ili fedha hizo zinazoletwa kwetu zilete tija,” amesema Toufiq.

Akizungumza kwa niaba ya madiwani, Mwenyekiti wa madiwani Mkoa wa Dodoma, Mwanaharusi Bata ameipongeza OSHA kwa kuendesha programu ya mafunzo hayo huku akiahidi kuwa wataifikisha elimu hiyo ya usalama na afya walioipata katika miradi mbalimbali inayotekeleza kwenye maeneo yao wanapotoka.

Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda akitoa neno la shukrani kwa madiwani wa viti maalumu wa Mkoa wa Dodoma walioshiriki katika mafunzo ya usalama na afya pamoja na zoezi la upimaji wa magonjwa yatokanayo na kazi lilifanyika katika ofisi za OSHA Dodoma.

Aidha, Mtendaji Mkuu wa OSHA, Khadija Mwenda amesema lengo kubwa la mafunzo haya ni kuwaelimisha madiwani hao kuhusu majukumu mbalimbali ya OSHA ili wanapopitisha na kusimamia miradi mbalimbali ya kimaendeleo waweze kushirikiana na OSHA katika kulinda nguvu kazi kwa kuboresha mifumo ya usalama na afya katika miradi hiyo.

“Mafunzo haya ni sehemu ya maelekezo ya Ofisi ya Waziri Mkuu na tutahakikisha tunaendelea kutoa elimu na kuyafikia makundi mbalimbali na moja wapo ni hili la watunga sera ili inapotokea wanakaa katika mabaraza ya kupitisha miradi basi waangalie miradi hiyo kama imekidhi viwango vya usalama na afya kama sheria husika inavyo elekeza,” alisema Mwenda.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img