21 C
New York

Mwandishi Gazetini kuwania tuzo EJAT

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Mwandishi Faraja Masinde kutoka tovuti ya www.gazetini.co.tz inayo chini ya Gazetini Communications ni kati ya waandishi wa habari 91 waliopitishwa na jopo la majaji wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari (EJAT) kuwania tuzo hizo ambazo zinatarajiwa kufanyika Julai 22, Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mapema leo Juni 23, 2023 akitangaza wateule hao jijini Arusha Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi EJAT 2022, Kajubi Mukajanga amesema waandishi 91 wameteuliwa kati ya 728 waliowasilisha kazi zao.

Amesema kati ya hao 36 wanaandikia magazeti, 27 mitandao ya kijamii na 15 ni kutoka redioni na wanaotokea kwenye runinga ni 15.

“Katika wateule wote 44 ni wanawake ambapo 16 kutoka kwneye magazeti, 12 kutoka mitandao ya kijamii, sita kutoka katika redio na 10 ni runingani, wateule wanaume jumla yao ni 47,” amesema Kajubi.

Aidha, kwamujibu wa Kajubi, mgeni rasmi katika kilele cha tuzo hizo atakuwa Jaji Othman Chande ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Haki Jinai.

Tangu kuanzishwa kwa tovuti ya gazetini www.gazetini.co.tz mwaka 2021, hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa mwandishi wake kuingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Tovuti ya gazetini iliyoasisiwa Dar es Salaam, Tanzania imekuwa ikichapisha maudhui yake kwa mfumo wa sanifu (visual, infographics) ikijikita katika jamii ambapo imeendelea kukua siku hadi siku ikiwamo mitandao ya kijamii ya https://www.instagram.com/gazetininews/ Twitter: https://twitter.com/gazetini?t=7L9NQHsyF85sXY2qRFZT6A&s=09 na Facebook.com/gazetini Tanzania.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img