1.4 C
New York

Infographic| Tunachofahamu kuhusu ndege mpya ya Boeing 767-300F

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Juni 3, 2023 Tanzania imepokea ndege ya kwanza ya mizigo aina ya Boeing 767-300F, ni wazi kuwa hatua hiyo itachochea kukuza na kulitangaza zaidi Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) na kuondoa changamoto ya usafirishaji mizigo kwa wafanyabiashara na wakulima nchini ambao wamekuwa wakiagiza na kusafirisha bidhaa mbalimbali nje ya Tanzania.

Aliyeongoza mapokezi ya ndege hiyo ya kisasa alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan yaliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julias Nyerere(JNIA) jijini Dar es Salaam.

Kulingana na taarifa ya ATCL, ndege hiyo ina uwezo wa kubeba tani 54 za mizigo huku ikiwa na uwezo wa kusafiri hadi saa 10 bila kutua kuongeza mafuta.

Kwa sasa ATCL imefikisha jumla ya ndege 13, ikiwa ni ndege moja zaidi mbele ya Shirika la Ndege la Rwanda(RwandAir) lenye ndege 12. Aidha, Rais Dk. Samia ameahidi kufanyia kazi ombi la ATCL la kuomba kuongezewa ndege nyingine ya mizigo ili kuwezesha shirika hilo kuweza kutanua mbawa zake katika sekta ya usafirishaji. Zaidi angalia usanifu wetu.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img