4.1 C
New York

Chart| Halmashauri 10 zilizozima Posi kwa muda mrefu

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Angellah Kairuki amesema wakurugenzi wa halmashauri ambao watashindwa kufikia malengo ya ukusanyaji mapato, wataondoka kwenye nyadhifa zao hizo.

Juni mosi, 2023 akizungumza jijini Arusha wakati wa kufunga Mkutano Mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Kairuki alionya kuwa baadhi ya halmashauri nchini zikiongozwa na Jiji la Dar es Salaam, Manispaa ya Kinondoni na Ubungo, wameshindwa kutoa leseni za biashara kwa wahitaji, na kusema jambo hilo linaweza kuzikosesha halmashauri mapato.

“Tutapataje pesa kama hatutoi leseni. Halmashauri haiwezi kupata mapato kama hakuna watu wanaofanya biashara na baadhi ya halmashauri ikiwemo Jiji la Dar es Salaam hawatoi leseni kwa baadhi ya wafanhabiashara wanaohitaji leseni hizo. Mkurugenzi ambaye atashindwa kufikia malengo ya ukusanyaji mapato hatavumilika,” alinukuliwa Kairuki.

Kwa mujibu wa Kairuki, baadhi ya halmashauri hazipeleki benki fedha mbichi jambo hilo linasababisha halmashauri kupata matatizo ikiwemo hoja za ukaguzi na kuagiza fedha zote mbichi zipelekwe benki.

Halmashauri 10 kinara kwa kusima posi

Akizugumzia mashine za ukusanyaji mapato (Posi) amesema kuwa halmashauri 10 zimeonekana kuzima posi kwa muda mrefu, ikiwemo Mbeya Jiji posi 124, Dodoma Jiji posi 121, Temeke posi 95, Kinondoni posi 88,Tunduma posi 84, Iramba posi 81, Dar es Salaam Jiji posi 77, Mbarali posi 74, Makete posi 72 na Muleba posi 72.

“Hizi ni halmashauri chache tu 10 ambazo nimezitaja na siyo kwamba wengeni hawazimi posi hivyo basi naomba niwambie kwamba kila mmoja awajibike kwasababu suala hili halitavumilika nendeni mkajipange,”amesema Kairuki na kuongeza kuwa:

“Unapokuwa kiongozi na wewe mwenyewe ukakosa maadili kwa kweli mnajiweka katika mazingira mbaya nendeni mkafanye kazi mkaheshimiane, kila moja akajua mipaka yake ya kazi,” amesema Kairuki.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img