4.1 C
New York

Chart| SADC inavyoinufaisha Tanzania

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Kulingana na Ripoti ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara ya mwaka 2023, inaonyesha kuwa kumekuwa na ongezeko la bidhaa za Tanzania zinazouzwa katika soko la la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Takwimu zinaonyesha kuwa Mwaka 2022, thamani ya bidhaa zilizouzwa katika soko la SADC ilikuwa ni dola za Marekani milioni 1,802.2 ikilinganishwa na dola za Marekani milioni 1,303.4 mwaka 2021. Hiyo ni sawa na ongezeko asilimia 38.2.

Akiwasilisha makadirio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/24 Mei 4, 2023 bungeni jijini Dodom,Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk. Ashantu Kijaji alibainisha kuwa ongezeko hilo lilitokana na kuongezeka
kwa uuzaji wa bidhaa mbalimbali katika soko hilo.

“Bidhaa zilizouzwa kwa wingi ni pamoja na madini, pamba, chai, parachichi, kahawa, vigae, vyandarua, saruji, sabuni na mafuta ya kupaka,” alisema Dk. Kijaji.

Zaidi angalia chart yetu kuangalia mwenendo wa mauzo hayo kwa miaka 10.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img