8.5 C
New York

Chati| Sababu za kushuka kwa ufaulu shule kuu ya Sheria Tanzania

Published:

Na, Anoth Paul, Gazetini

Kwa mujibu wa Matokeo mwaka 2022 ni asilimia 4.1 tu ya wahitimu wamefaulu.

Ndoto ya wanafunzi 633 katika Shule Kuu ya Sheria iliyoko jijini Dar es Salaam ilikuwa ni kuwa Mawakili na hata Wanasheria licha ya kwamba wote hao hutokea vyuo vikuu tofauti nchini na hata nje ya nchi.

Hali imekuwa tofauti katika shule hiyo licha ya idadi ya wanafunzi wengi kufanya mitihani ya uwakili kila mwaka, kwa muujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye gazeti la Mwananchi kupitia ukurasa wake wa Instagram ilieleza kuwa katika idadi ya wanafunzi 633 waliofanya mtihani wa uwakili kwa mwaka 2021/2022 ni 26 tu ndiyo walifaulu sawa na asilimia 4.1, huku wanafunzi 342 wakitakiwa kurudia baadhi ya masomo na wengine 265 sawa na asilimia 41.9 wakishindwa kufaulu na kulazimika kukatishwa masomo yao.

Matokeo haya yanaakisi kuwepo kwa ufaulu usioridhisha katika shule hiyo pia tutazame matokeo ya mwaka 2020/2021 wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 635 na waliofaulu walikuwa ni 26 pekee ambayo ni sawa na asilimia 4.0% huku idadi ya wanafunzi 609 sawa na asilimia 95% wakishindwa na wengine kulazimika kurudia masomo. 

Sehemu ya Majengo ya Chuo cha Sheria.

Pia kwa miaka ya masomo 2018/2019 na 2019/2020 kati ya wanafunzi 2,662 waliofanya mtihani, ni wanafunzi 445 sawa na 16.72% walifaulu na 1,611 (60.53) walirudia mtihani wakati 606 (22.76) walifeli. Na hiki ndicho kiliifanya Serikali kupitia kwa Waziri wa Katiba na Sheria nchini, Dk. Damas Ndumbaro  kuunda vikosi vya kuchunguza sababu za ufaulu duni katika shule hii.

Hebu tutazame takwimu za ufaulu wa mitihani kwa asilimia wa mwaka 2021/2022 kwa baadhi ya nchi Afrika kwa muujibu wa Gazeti la Daily Monitor kupitia hii chati. Ufaulu huu umekuwa changamoto inayowapelekea baadhi ya wanafunzi kuchukua hatua za kuzishitaki shule zao ili wapate haki zao.

Baadhi ya mawakili kupitia mjadala wa ‘space’uliokuwa ukiendeshwa na Kampuni ya Mwananchi Communications wamependekeza kuongezwa muda wa kusoma Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo Tanzania (LST) ili kukabiliana na changamoto ya matokeo mabovu kwa wanafunzi.

Kando ya hilo, wamependeza kufanyika tathmini ya wanafunzi wanaojiunga na taasisi hiyo kwa madai baadhi ya wanaojiungani kwa kuwa wana uwezo wa kulipa ada na kuchukulia taaluma ya sheria kama suala rahisi.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img