1.7 C
New York

Visual| Geita inavyoitikia Uzazi wa Mpango

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Mkoa wa Geita ni kati ya mikoa 31 ya Tanzania. Umepakana na Kagera upande wa Magharibi, Shinyanga upande wa Kusini na Mwanza upande wa mashariki.

Kama inavyofahamika kuwa Geita imekuwa ni kati ya mikoa michache nchini Tanzania ambayo imekuwa ikitoa elimu ya uzazi wa mpango kwa wanandoa.

Hatua hiyo hakuna shaka kwamba imekuwa na mafanikio makubwa. Hii ni kufuatia kuwapo kwa takwimu ambazo zinabeba mafanikio ya mpango huo.

Daniel Sinda ni Mratibu wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto mkoa wa Geita ambaye anabainisha kuwa katika kipindi cha miaka mitano kuanzia 2017 hadi 2021 jumla ya wanawake 17,616 wamefunga uzazi ikiwa na maana kwamba hawatahitaji watoto tena.

Huduma hiyo wameipata katika moja ya vituo 165 vya afya vilivyoko mkoani humo.

Sinda anabainisha kwamba kumekuwa na mwitikio mkubwa wa matumizi ya huduma ya uzazi wa mpango mkoani humo.

“Kwa mujibu wa takwimu mwaka 2017 pekee takribani wanawake 6,210 walijitokeza kupata huduma ya kufunga kizazi kwa mkoa mzima. Kwa mwaka 2018 walijitokeza wanawake 4,373.

“Aidha, mwaka 2019 walijitokeza wanawake 2,179, mwaka uliofuata wa 2020 walikuwa wanawake 2,928 na mwaka 2021 walikuwa wanawake 1926,” anasema Sinda.

Kufuata uzazi wa mpango

Pamoja na wanawake hao 17,616 kuchagua kufuanga buzazi, pia wapo ambapo wameamua kutumia uzazi wa mpango kwa ajili ya kujipa nafasi ya kulea watoto na kutimiza malengo waliyojiwekea.

Sinda anabainisha kuwa kundi hilo pia ni kubwa hatua ambayo inaashiria kufikiwa na elimu ya uzazi wa mpango kwa wanawake walio wengi mkoani humo.

Anasema kwa mwaka jana wa 2021 wanawake 8,439 walifuata njia ya uzazi wa mpango ya kutumia vidonge.

“Mbali na hao, mwaka jana pia (2021) wanawake 27,296 walijitokeza kupanga uzazi kwa kutumia njia ya sindano, wengine 42,488 walipanga uzazi kwa njia ya vipandikizi kwa maan ya kijiti na wanawake 12,151 walichagua kupanga uzazi kwa njia ya kitanzi,” anasema Sinda.

Tathimini

Kwa mujibu wa Sinda, tathimini inaonyesha kuwa wanawake wengi wanapendelea kutumia zaidi njia ya vipandikizi nakwamba hadi sasa huduma ya uzazi wa mpango inapatikana katika vituo vya afya 165 mkoani Geita na kwamba inaendelea kufikishwa kwenye maeneo mengine kupitia kampeni ya Mkoba.

Martha Samwel mkazi wa miti mirefu mjini Geita ni miongoni mwa waliofunga uzazi ambapo anasema kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo ili kupata muda wa kufanya shughuli za ujasiriamalia na kulea watoto alionao.

“Mimi nina watoto wanne, sioni haja ya kuongeza wengine wakati hawa niliona wenyewe wananitoa jasho, nikiongeza nitawaleaje mie, acha nipumunzike ili niweze kufanya mambo mengine,” anasema Martha.

Martha anakiri kuwa hatua hiyo imemupa nafasi ya kuwahudumia watoto wake kwa ufasaha na kuwawezesha kupata mahitaji ya msingi kwa maana ya malazi, mavazi na chakula.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img