21 C
New York

Infographic| Hatua zilizopigwa Sekta ya Mifugo na Uvuvi

Published:

Sekta ya Mifugo ni miongoni mwa maeneo ambayo Tanzania imekuwa ikiyatumia katika kuingiza fedha za kigeni ikiwamo pia utoaji wa ajira kwa Watanzania.

Hata hivyo, pamoja na sekta hiyo kufanikiwa kupiga hatua kadhaa lakini bado haijafikia mafanikio yanayoridhisha.

Kutokana na kuchechemea huko ndiyo sababu ya Serikali inawaza kubadili mbinu ya uendeshaji kwa maana ya kuimarisha mfumo wa sasa na kuhakikisha inaendeshwa kibiashara ili kuleta tija kwa Wafugaji na Taifa kwa ujumla.

Aidha, serikali inapanga kuhakikisha kuwa rasilimali za uvuvi zinasimamiwa ipasavyo ili kuwa na uvuvi na ukuzaji viumbe maji endelevu, maendeleo ya viwanda, ukuaji wa kipato cha mtu mmoja mmoja na Pato la Taifa kwa ujumla.

Kwa mujibu wa Waziri wa Wizara hiyo,Mashimba Ndaki, sekta ya Uvuvi ni mwongoni mwa sekta za uzalishaji mali ambayo ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo ya usimamizi na uratibu wa uendeshaji wa shughuli za uvuvi nchini.

Hali ilivyo nchi kwasasa

Kg 8.5- Kiwango cha ulaji wa samaki kwa sasa nchini kwa mtu kwa mwaka, ikilinganishwa na kiwango kinachopendekezwa na Shirika na Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (Kg 20.3)
Nchi zinazonunua nyama Tanzania: Oman, Kuwait, Qatar, na Vietnam.
Sh Tril. 1.4- Kiasi cha fedha kinachotarajiwa kutumika katika ujenzi wa Bandari ya Uvuvi kupitia Mtaalam Mwelekezi ambaye ni Kampuni ya M/S Sering Ingegneria ya Italia.
Tani 750,000 – Kiwango cha mahitaji ya samaki kwa mwaka hapa nchini
Tani 496,390 – Kiwango cha samaki kinachozalishwa nchini, ambapo ni sawa na upungufu wa tani 253,615.
2026- Mwaka ambao matarajio ya Wizara ni kuona ulaji wa samaki kwa Watanzania unafikia Kg 10.5 kwa mwaka.
30%- Kiwango cha upotevu wa mazao ya uvuvi baada ya kuvunwa, huku lengo likiwa ni kufikia asilimia 10.
13,593- Idadi ya vyombo vya uvuvi vinavyotumia injini, ambapo lengo ni kufikia 25,000 ifikapo mwaka 2015.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img