21 C
New York

Infographic|Hali ilivyo watoto wanaougua saratani ya jicho nchini

Published:

TATIZO la Ugonjwa wa Saratani ya Macho (Retinoblastoma) kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano limeanza kushamiri mkoani Mbeya kutokana na idadi ya watoto wanaobainika kuugua ugonjwa huo kuongezeka.

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya macho katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya, Dk. Fariji Kilewa alisema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita, zaidi ya watoto 23 wenye umri wa kati ya  miaka sifuri hadi  mitano wamebainika kuugua ugonjwa huo.

Alisema tatizo hilo linazidi kuwa kubwa kutokana na wazazi wengi kutojua dalili za ugonjwa huo na hivyo kushindwa kuchukua hatua za haraka kuzuia au kutibu ugonjwa huo kwa watoto wanaougua.

“Katika kipindi cha kuanzia 2015 hadi Septemba mwaka huu tumebaini watoto 23 ambao tayari wamepata maambukizi ya ugonjwa huu, hali hii sio nzuri ikilinganishwa na miaka ya nyuma ambapo watoto wanaokutwa na ugonjwa hu ilikuwa ni nadra sana kuwapata,” alisema Dk. Fariji.

Akizungumzia chanzo cha ugonjwa huo, Dk. Fariji alisema miongoni mwa sababu za watoto kuugua saratani ya macho ni pamoja na mabadiliko ya vinasaba vya wazazi.

Akizungumzia dalili za ugonjwa huo, Dk. Kilewa, alisema kuwa punde tu mtoto anapozaliwa anaweza kuhisiwa kuwa ataugua saratani ya macho endapo ataonekana macho yake yanang’aa nyakati za usiku kama yalivyo macho ya paka.

Aidha alisema hospitali hiyo unaendelea kutoa huduma za upasuaji wa macho kwa makundi yote  na kwamba katika kuhakikisha huduma hiyo inamfikia kila mwenye uhitaji wanafanya kampeni za mara kwa mara kuhamasisha  upimaji katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya.

Aliongeza kuwa pia  Serikali kupitia Wizara ya Afya imeajiri madaktari wa macho katika kila Wilaya za Mkoa huo licha ya kuwa bado wahudumu  ni wachache hivyo anaiomba Serikali kuendelea kuajiri wataalam hao.

Alisema endapo  hatua hazitachukuliwa haraka, utatokea uvimbe ndani ya jicho lenye dalili hizo na uvimbe huo utasambaa mwili mzima ambapo itafikia hatua ambapo kutakuwa hakuna tena tiba na mtoto huyo atapoteza maisha.

Baadhi ya wazazi mkoani Mbeya walisema hawa uelewa juu ya dalili za  ugonjwa wa saratani ya jicho kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano.

Mmoja wao Lupakisyo Mathayo alisema katika jamii yake alishahudia mtoto mdogo kuwa na makengeza lakini hakujua ni moja ya dalili za Saratani ambapo alipoteza maisha.

Alisema elimu ya kutambua dalili na athari za ugonjwa huo ziendelee kutolewa katika jamii ili iwe rahisi kufika katika vituo vya kutolea huduma na kuokoa uhai wa mtoto.

Kwa mujibu wa Takwimu za Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee Watoto  (WAMJW ) kwa mwaka 2017 jumla ya watoto 149 waligundulika kuwa na Saratani  ya Macho (Retinoblastoma) 2018 watoto  137, 2019 watoto 150 na 2019 hadi oktoba 90.

Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto hususani Saratani kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili MUHAS, Dk. Anna Sanyiwa alisema  Saratani hiyo inasababishwa na uvimbe  unatokea katika seli za pazia ya jicho na retina zinaanza kuzalisha bila mpangilio na kusababisha uvimbe.

Chanzo hitilafu kwenye vina saba vya Seli za mwanadamu ikitokea hiyo inashindwa kuzuia seli zisizaliane bila mpangalio na kutoa uvimbe

Alisema kwa kipindi cha mwaka 2015 katika wadi ya watoto Hospitali ya Muhimbili jumla ya watoto 360 kati yao 76 saratani ya jicho 20 asilimia. Mwaka 2016 wagonjwa  418  kati yao 71 waliugua saratani ya jicho na 75  satarani ya damu huku akisisitiza kuwa hitilafu ya vina saba wakati mtoto yuko  tumboni huchangia tatizo hilo.

“Kuna watoto  wengine hutokea hupata ugonjwa huo bila vina saba  unashangaa anagua jicho moja lakini kwa kawaida  anayeugua macho yote mawii husababishwa na  vina saba hususani wanaoana ndugu wa karibu”, alisema Dk. Sanyiwa.

Aliongeza kuwa dalili za mapema za ugonjwa huo ni  weupe kwenye macho, mtoto akifungua macho hususani usiku unaona jicho linang’aa  au makengeza na kwamba ni  ngumu kutambua mapema kwa sababu mtoto huwa vizuri bila kuonyesha dalili zozote za homa kushindwa kula au kutapika.

Alidai ugonjwa unavyoendelea ndivyo uvimbe ndani ya jicho unakua na inapofikia dalili za maumivu jicho kuwa jekundu ambapo uvimbe hujitokeza nje ni dalili za mwisho kabisa.

Kuhusu matibabu alisema hutegemea mgonjwa amekuja katika hatua gani kama ni makengeza kuna dawa za mishipa na mionzi inawekwa kwenye jicho ili kuua ule uvimbe na jicho halitolewi.

Na kwamba uvimbe mkubwa ambao husababisha jicho kutokuona matibabu yake ni kutoa ili kuzuia usisambae na kumnusuru  mtoto asipoteze maisha kwa kutumia mashine maalumu.

Pamoja na yote hayo lakini jamii bado haijakubalika kwamba endapo mtoto akifikia hatua za mwisho za kutolewa jicho  ili kunusuru maisha yake wazazi wanaahirisha hii ni dhana ambayo inapaswa kubadilishwa familia haikubali ushauri wa kutoa jicho kwa mgonjwa,”alisema Dk. Sanyiwa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img