18.6 C
New York

Mjumbe Maalum wa Rais Samia, Jakaya Kikwete akutana na Rais wa Burkina Faso

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais mstaafu Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, amehitimisha ziara yake kwa kukutana na Rais wa Burkina Faso, Captain Ibrahim Traoré, katika mkutano uliofanyika Aprili 17, 2025 jijini Ouagadougou.

Mkutano huo ulihudhuriwa na maafisa waandamizi kutoka Serikali zote mbili, ambapo, Kikwete aliwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Rais Samia. Akizungumza katika mkutano huo, Kikwete alimshukuru Rais Traoré kwa kumpokea na kumpa fursa ya kuwasilisha ujumbe wa kiongozi wa Tanzania.

“Rais wangu amenituma nije kuwasilisha ujumbe maalum kwako na nimefurahi kwa ukarimu ulionionesha na leo umeupokea rasmi,” alisema Kikwete.

Aidha, Kikwete aliwasilisha salamu za Rais Samia zenye kuhimiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano baina ya nchi za Afrika, hususan katika kubadilishana uzoefu, maarifa na mbinu bora za kuendeleza rasilimali za bara hilo kwa faida ya wananchi wake.

Ujumbe huo umeelezwa kuwa ni sehemu ya juhudi endelevu za Tanzania kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia, kiuchumi na kijamii na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, ili kuhimiza mshikamano na maendeleo ya pamoja barani Afrika.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img