2.9 C
New York

Watoto wahamasishwa kutunza Amani kupitia sanaa

Published:

Na Mwandishi Wetu, Gazetini

Mratibu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania na Mratibu wa Amani Duniani wa Taasisi ya Kimataifa ya Amani ya Wanawake (IWPG), Fatuma Fredrick, amewasihi Watanzania kuendeleza juhudi za kuimarisha amani nchini.

Akizungumza Julai 14, 2024, wakati wa hafla ya utoaji tuzo za michoro ya kuhamasisha amani kwa watoto, jijini Dar es Salaam, Fatuma alisema ni muhimu kuhimiza amani kwa watoto tangu wakiwa wadogo.

“Tuna bahati kuwa na amani Tanzania. Ni wajibu wetu kuhakikisha tunahimiza amani kwa vizazi vijavyo,” alisema Fatuma. Mashindano ya IWPG yanalenga kudumisha amani, kupendana, na kuvumiliana.

George Magambo kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania alisifu juhudi za IWPG, akisema zitachukuliwa na kufundishwa shuleni ili kujenga utamaduni wa amani. Ndendeksye Mwayohojo, mshindi wa pili kutoka Shule ya Sekondari ya Alpha, alichora umbo la dunia na njiwa, akisisitiza amani duniani.

Wakili Jackline Kibaha, mzazi wa Ndendeksye, alisema mashindano haya yanapanda mbegu ya amani kwa watoto. Mona Theobad, Mwakilishi wa Meneja wa IWPG Tawi la Dar es Salaam, alisema mashindano yameonyesha umuhimu wa amani kwa watoto, na walioshinda walipatiwa zawadi mbalimbali.

“Tunaendelea kuhakikisha dunia inakuwa salama kwa kuhamasisha amani,” alisema Mona. Mashindano ya mwaka huu yalilenga kuhimiza nchi zinazopigana vita kuachana na vita na kudumisha amani.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img